Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Azam fc. Kila la kheri wana 'Lambalamba'.
MABINGWA watetezi wa Tanzania, Azam fc usiku wa leo majira ya saa mbili usiku wanakabiliana na Al Merrick katika mechi ya marudiano ya ligi ya mabingwa Afrika itayopigwa mjini Khartoum.
Meneja wa Azam fc, Jemedari Said Mzumari amesema kwa maandalizi waliyofanya wanaamini watafanya vizuri.
"Wachezaji wote wapo katika sura nzuri, jana tulifanya mazoezi vizuri, leo tunapambana kwa namna yoyote ile kushinda mechi huu ngumu kwetu". Amesema Jemedari.
Nao wachezaji wa Azam, Himid Mao Mkami na Frank Domayo wamezungumzia maandalizi yao.
"Vitu vyote vinavyotokea ni kawaida katika soka la Afrika, walimu walituambia mambo hayo yatakuwepo, tumejiandaa vizuri na tunaamaini tunashinda". Amesema Himid Mao.
"Unapocheza na waarabu fitina zipo nyingi, lakini tumejiandaa na walimu walitujenga mapema kisaikolojia, leo tutapambana kufa na kupona". Amesema Frank Domayo.
Naibu waziri wa Habari, vijana, utamaduni na michezo wa Tanzania, Juma Nkamia amewatambelea Azam fc nchini Sudan na amewataka kupambana kwa hali na mali ili kushinda mechi hiyo.
"Azam ni timu, lakini inawakilisha Tanzania. Wimbo wa Taifa wa Tanzania ndio utakaopigwa, lazima Watanzania tuwaunge mkono. Wachezaji jitumeni sana ili mpata matokeo. Mna faida ya magoli mawili, yalindeni na tafuteni mengine". Amesena Nkamia.
Ili kusonga mbele Azam fc wanahitaji sare ya aina yoyote ile au kutofungwa zaidi ya goli 1-0. Hii inatokana na matokeo ya 2-0 waliyopata Azam Complex, februari 15 mwaka huu.
Mabao hayo yalifungwa na Didier Kavumbagu na John Boco 'Adebayor".
Wakati huo huo wawakilishi wengine wa Tanzania, Yanga, jana wafanikiwa kusonga mbele raundi ya pili ya kombe la shirikisho baada ya kuwatoa BDF XI kwa wastani wa magoli 3-2.
Yanga walifungwa 2-1 jana mjini Gaborone, lakini kwa kuwa walishinda 2-0 uwanja wa Taifa, walifuzu raundi inayofuata.
0 comments:
Post a Comment