Halmashauri ya jiji la Mbeya ambayo ndio mmiliki wa timu ya Mbeya City football Club ilikutana na bodi ya Michezo ya jiji inayosimamia uendeshaji wa timu leo tarehe 23.02.2015 kujadili muenendo mzima wa mchezo wa timu yetu dhidi ya Young African uliochezwa tarehe 22.02.2015 pamoja na matokeo yake.
Katika kikao hicho,mmiliki pamoja na bodi yake walipitia taarifa na rejea ya mchezo husika na kugundua mambo yafuatayo:
1. Kiufundi timu ilicheza vizuri na kwa kiwango cha hali ya juu ikilinganishwa na wapinzani wetu, ila ilikosa kitu kimoja tu nacho ni ushindi.
2. Mchezaji David Abdallah Buruhani ambaye alikuwa golikipa katika mchezo huo alifanya makosa binafsi na ya makusudi yaliyoigharimu timu kukosa ushindi katika mchezo husika. Makosa ya mchezaji huyu katika mchezo huo yalikuwa yanafanana na baadhi ya makosa ambayo alishawahi kuyafanya huko nyuma na kusahihishwa.
Baada ya kupitia rejea kadhaa ilibainika kuwa makosa mengi ya aina hii yamekuwa yakifanyika katika baadhi ya mechi hasa zinazohusisha timu zenye ushawishi. Mazingira mazima ya makosa yote hayo yamezingirwa na mashaka makubwa ambayo ni vigumu kujiweka mbali nayo akiwa kama mhusika mkuu.
Baada ya uchambuzi wa nyaraka mbalimbali na rejea zake, mmiliki ambaye pia muajiri wa mchezaji husika amemsimamisha na kumuondoa kikosini mpaka hapo atakapomjulisha vinginevyo.
Halmashauri ya jiji la Mbeya imesikitishwa na mazingira mazima yaliyojitokeza ya kupoteza mchezo huo,ni kweli mchezo wa mpira wa miguu ni mchezo wa makosa ila aina gani na mazingira yapi ya kosa husika ni changamoto na kushinda na kushindwa ni sehemu ya mchezo ila umeshindwa je na katika mazingira yapi ni changamoto kubwa zaidi.
Dismas Ten
(signed)
AFISA HABARI
MCC FC
0 comments:
Post a Comment