Thursday, February 5, 2015

GUINEA ya Ikweta ina uwezo wa kukabiliana na presha ya safu ya ushambuliaji ya Ghana katika mechi yao ya nusu fainali ya Afcon inayopigwa leo usiku na hawataogopa hata kama Asamoah Gyan atakuwa fiti, amesema kocha Esteban Becker.
Mshambuliaji wa Ghana, Gyan hana uhakika wa kucheza kutokana na majeruhi aliyopata baada ya kugongana na kipa wa Guinea Naby Yattara katika ushindi wao wa mabao 3-0 robo fainali.
"Wachezaji hawana majina makubwa sana , wanacheza ligi daraja la pili na tatu, lakini wamecheza dhidi ya wachezaji wakubwa kabla. Hata wale ambao tunacheza nao hapa Guinea ya Ikweta wamecheza dhidi ya wachezaji wakubwa kabla.," Becker amewaambia waandishi wa habari.
"Licha ya hili, mabeki wangu wamecheza dhidi ya Fernando Torres kwa Hispania, tena mabingwa wa dunia. Hata katika mashindano hato wamecheza na wachezaji wakubwa"

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video