George Kavila (kushoto) akikabiliana na Elias Maguli desemba 26 mwaka jana Simba wakichapwa 1-0.
Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaam,
Malengo makubwa ya Kagera Sugar msimu huu ni kuwa miongoni
mwa klabu tatu ambazo zitamaliza ndani ya nafasi tatu za juu. Kagera ambayo kwa
sasa wanautumia uwanja wa Kambarage, Shinyanga kama uwanja wao wa nyumbani
kufuati uwanja wa Kaitaba kuwa katika matengenezo makubwa. Ikiwa katika nafasi
ya tatu katika msimamo timu hiyo ya Bukoba itacheza na ‘ wenyeji halisi wa
Kambarage Stadium’ Stand United katika mchezo wa ligi kuu Bara kesho Jumamosi.
Mchezo huo unaraji kuwa mkali kwa kuwa Stand imejiimarisha
na kushinda michezo kadhaa ukiwemo ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba SC wiki
iliyopita. “ Kila kitu kinakwenda vizuri, tuna hali ya kupambana. Tayari
tumecheza michezo migumu msimu huu na pengine gemu dhidi ya Ruvu Shooting na
JKT Ruvu ndizo zilikuwa ngumu zaidi upande wetu msimu huu lakini kiujumla ligi
ni ngumu na hatujachoka kupambana” anasema George Kavila mchezaji wa Kagera
Sugar kwa msimu wa tano sasa.
Kagera imekuwa na kawaida ya kuanza msimu vizuri lakini
humaliza ligi vibaya kiasi cha kufanya imalize katika nafasi za nne msimu wa
2012/13 na nafasi ya tano msimu wa 2013/14 licha ya kuwa na matokeo mazuri
katika michezo ya mwanzo. Uzoefu mdogo umekuwa ukitajwa kama sababu ya kufanya
vibaya kwa timu hiyo mwishoni mwa msimu na hivyo hushindwa kutimiza malengo
yake.
“ Tubataka kuendelea kucheza mechi zetu na kupata matokeo
mazuri mazuri, hatutaki kuangalia timu nyingine zinafanya nini ama timu gani
inacheza na nani. Tutazidi kuwa bora msimu huu mpaka siku ya mwisho na kutimiza
malengo yetu ya kuingia ‘top3’. Siku zote tunapambana huku tukizipa heshima
kubwa klabu pinzani, hakuna timu ambayo tunaiogopa” anasema mchezaji huyo
ambaye kwa mara ya kwanza alicheza ligi kuu Tanzania Bara mwaka 1998
aliposajiliwa na Coastal Union ya TaNGA. Kavila amewahi kuzichezea klabu za
Coastal, 1998-2004, Twiga Sport, 2004-05, Polisi Moro, 2006, Moro United na
tangu mwa ka 2009 amekuwa katika klabu ya Kagera Sugar.
0 comments:
Post a Comment