Mosoti wakati alipokuwa Simba
Na Berther Lumala
SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa (FIFA) limeipa
klabu ya Simba siku 30 kuanzia jana kuhakikisha inamlipa beki wa kati Donald
Mosoti dola za Marekani 13,800 kutokana na kusitisha mkataba wa Mkenya huyo.
Maamuzi hayo yalitolewa na FIFA jana Alhamisi
kupitia jopo la majaji wa Kitendo chake cha Usuluhishi na Uamuzi, Simba
ikitakiwa kulipa kiasi hicho cha fedha kwa beki huyo baada ya kukiuka masharti
ya kimkataba.
Katika barua ya FIFA ambayo mtandao huu uliiona
jana ikiwa na anuani ya FAX +4143/222 77 55, iliyotumwa kwenda kwa mchezaji na
upande wa Tanzania (Shirikisho la Soka nchini – TFF),imeamuliwa kuwa, Simba
inapaswa kumlipa mlalamikaji, Donald Mosoti Omanwa, ndani ya siku 30 kuanzia
tarahe ya kupokea maamuzi hayo (jana) kama ilivyoamuliwa na jopo la
majaji watatu; Thomas Grimm (Uswisi), Eirik Monsen (Norway) na Zola Majavu
(Afrika Kusini).
Kutotekeleza maamuzi hayo kutaifanya klabu
husika (Simba) kufikishwa mbele ya Kamati ya Nidhamu ya FIFA kwa kuzingatia
uamuzi na utaratibu wa kawaida wa shirikisho (FIFA).
USD 13 800
Katika barua hiyo, Simba inatakiwa kumlipa
Mosoti ndani ya siku 30 kuanzia jana, dola 13,800 na penalti ya asilimia tano
(5%) ambayo ni dola za Marekani 600 kutokana na kumharibia mipango yake kisoka
kuanzia Decemba 12, 2013 hadi siku ambayo malipo yatafanyika.
Sehemu ya maamuzi hayo yaliyosainiwa na Katibu
Mkuu wa FIFA, Jerome Valcke, yanasomeka: Wahusika wanapaswa kumlipa mlalamikaji
ndani ya siku 30 kuanzia tarehe ya kupokea maamuzi haya, fidia ya kuvunja USD
13 800 pamoja na 5% ikiwa ni penalti kuanzia16 Septemba 2014 hadi tarehe ambayo
malipo hayo yatafanyika.”
KUVUNJA MKATABA
Simba ilimtema nyota huyo wa zamani wa Simba
wa Nairobi City na Gor Mahia, zote za Ligi Kuu ya Kenya (KPL) Agosti 2014 akiwa
amebakisha mwaka mmoja na miezi mitatu katika mkataba wake bila kumpa taarifa
zozote juu ya kumwacha huku jitihada zake za kulimaliza suala lake kwa amani
zikishindwa kuzaa matunda.
Mchezaji huyo kupitia wakili wake, Mwanasheria
Felix Majani aliamua kulifikisha FIFA suala hilo baada ya kuzungushwa na
uongozi wa Simba jijini Dar es Salaam kwa muda mrefu.
Alikaribisha kujiunga na Tusker FC kulinda
kipaji chake wakati kesi hiyo ikishughulikiwa lakini ilikuwa ngumu kupata Hati
ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) hadi pale FIFA ilipoingilia na kuruhusiwa
kuitumikia klabu hiyo ya KPL msimu huu.
Mosoti alijiunga na Simba Desemba 2013 akitokea
Gor Mahia kwa ushawishi waaliyekuwa kocha mkuu wa Simba, Mcroatia
Zdravko Logarusic aliyefukuzwa pia.
Hii si mara ya kwanza klabu za Tanzania kuagizwa
zilipe mamilioni ya shilingi na FIFA kwani Yanga pia ilishawahi kuagizwa na
shirikisho hilo lenye mamalaka ya juu kisoka ulimwenguni kumlipa beki wa
kushoto Mkenya John Njoroge Sh. million moja
za Kenya baada ya klabu hiyo ya Jangwani kuvunja makataba wake kienyeji.
0 comments:
Post a Comment