Klabu ya Manchester United itashuka dimbani kuikabili timu ya Cambridge United katika mchezo wa marudiano kombe la FA.
Hii ni baada
ya kutoka sare ya bila kufungana katika mchezo wa kwanza uliochezwa
Abbey Stadium Nyumbani kwa Timu hiyo ya Daraja la Chini, Ligi daraja la
2.
Hii ni Mechi ya raundi ya 4 ya kombe la FA na Mshindi atatinga
Raundi ya 5 na kucheza na Mshindi kati ya Preston au Sheffield United
ambao nao wanarudiana leo Jumanne,huku mechi za Raundi ya 5 zikichezwa Wikiendi ya Februari 14 na 15.
Michezo mingine inayochezwa leo ni Fulham dhidi ya Sunderland, huku Sheffield United wakiwakabili Preston
Jumatano kutakua na mchezo mmoja ambapo majogoo wa jiji Liverpool watakua wakichuana vikali na Bolton Wanderers.
0 comments:
Post a Comment