Wakala wa Mshambuliaji wa klabu ya Manchester City na timu ya Taifa ya Bosnia Edin Dzeko, Irfan Redzepagic amesema mshambuliaji huyo huenda akajiunga na klabu mojawapo kati ya mabingwa wa ligi kuu nchini Uhispania Atletico Madrid au mabingwa wa Serie A Juventus Turin.
Hii ni baada ya mshambuliaji huyo kukosa namba katika kikosi cha kwanza cha Manchester City chini ya kocha Manuel Pellegrin, lakini pia ujio wa mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ivory Coast aliyekuwa anakipiga katika klabu ya Swansea City Wilfred Bonny aliyesajiliwa katika dirisha dogo la usajili mwezi January.
Redzepagic alisema licha ya kutowepo ofa yoyote iliyotumwa katika dirisha dogo la usajili na klabu yoyote ile, bado kuna uwezekano mkubwa mchezaji huyo kuondoka katika Ligi Kuu Nchini Uingereza.
"Dzeko ana miaka ishirini na nane sasa na anataka kucheza kwenye timu zenye upinzani mkubwa Barani Ulaya, na kama ataondoka Manchester City basi angependa kujiunga na klabu kubwa kama vile Juventus na Atletico Madrid,"Redzepagic aliliambia Gazeti la Fanatik
0 comments:
Post a Comment