Monday, February 2, 2015


Na Bertha Lumala, Dar es Salaam

Unamjua Dan Sserunkuma? Ni mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Kenya (KPL) akiifungia mabao 16 Gor Mahia na kuipa taji la pili mfululizo la ligi hiyo msimu uliopita kabla ya kujiunga na Simba SC msimu huu.

Mwenendo wake katika klabu hiyo mpya yenye mwendo wa kusuasua -- Simba -- umekuwa mbaya baada ya kushindwa kufunga hata bao moja katika mechi sita za Kombe la Mapinduzi 2015 visiwani Zanzibar.

Lakini, juzi straika huyo Mgandea alirejea katika makali yake baada ya kuifungia Siomba SC mabao yote mawili katika ushindi wao wa 2-1 dhidi ya maafande wa JKT Ruvu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Ushindi huo umeifanya Simba SC ifikisha pointi 16, tano nje ya janga la kushuka daraja baada ya michezo 12, wakati JKT inaendelea kuwa ya tatu ikiwa na pointi 18 sawa na Yanga SC walioko nafasi ya pili ambao leo jioni watakuwa wakipepetana na Ndanda FC ya Masaso, Mtwara Uwanja wa Taifa.

Sserenkuma alifunga bao la kwanza la Simba SC kwa shuti la karibu kutoka ndani ya eneo la hatari, dakika ya pili tu tangu kuanza kwa mchezo kutokana na pasi murua ya kiungo mshambuliaji Mganda Emmanuel Okwi, ambaye jana alirejea uwanjani baada ya kukosa mechi iliyopita waliyolala 2-1 dhidi ya Mbeya City Uwanja wa Taifa Jumatano baada ya kugongwa na kupoteza fahamu na beki wa kati wa Azam FC, Mzanzibar Aggrey Morris.

Sserunkuma kama ilivyokuwa mwanzoni mwa kipindi cha kwanza, alitumia dakika tatu tu kipindi cha pili kufunga bao la ushindi na lake la pili katika mchezo huo kufuatia krosi nzuri ya Mganda mwenzake, Okwi.

Lilikuwa bao la tatu katika mechi nne za Ligi Kuu kwa Sserenkuma ambaye alisajiliwa wakati wa dirisha dogo kuondoa ubutu katika safu ya ushambuliaji ya Simba SC baada ya Mrundi Amisi Tambwe kutoaminika kwa kocha aliyetimuliwa Mzambia Patrick Phiri.

Bao la kufutia machozi la JKT Ruvu inayonolewa na kocha wa zamani wa Yanga SC, Fred Felix Minziro lilifungwa na George Minja katika dakika ya  19 akiungnaisha kwa kichwa kikali mpira wa kona iliyochongwa na Iddi Mbaga.

Baada ya mechi hiyo, Kocha Mkuu wa JKT Ruvu, Minziro, alisema: "Tulikuwa na nafasi nzuri ya kushinda mechi ya leo (jana) kutokana na udhaifu mkubwa wa kikosi cha Simba lakini tumeponzwa na mabeki na viungo. Pasi za viungo wetu hazikuwa na uhakika wa kuwafikia washambuliaji. Pia kuliwa na 'poor marking' (ukabaji dhaifu) kwa mabeki wetu. Magoli yote mawili ni kwa sababu ya kutokaba vizuri."

Kocha Mkuu wa Simba SC, Mserbia Goran Kopunovic hakuzungumza na waandishi wa habari baada ya mechi hiyo, kinyume cha kanuni za Ligi Kuu za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) toleo la 2014.

Ushindi wa Simba SC wa juzi ni kisasi kwa JKT Ruvu kwa vile timu hiyo ilikifunga kikosi cha Mcroatia Zdravko Logarusic cha wekundu wa Msimbazi mabao 3-2 Uwanja wa Taifa katika mechi yao ya mwisho msimu uliopita.

Vikosi vilikuwa:
SIMBA SC: Ivo Mapunda, Kessy Ramadhani, Mohammed Hussein, Hassan Isihaka, Murshid Juuko, Thomas Mkude, Ramadhani Singano, Abdi Banda/ Awadh Juma (dk.88), Dan Sserenkuma, Ibrahim Ajib/ Simon Sserenkuma (dk.67), Emmanuel Okwi.

JKT RUVU: Benjamin Haule, Ramadani Shamte, Napho Zubeir, Renatus Moris, Mohammed Faki, George Minja, Ally Bilali/ Issa Kanduru (dk.68), Naftar Nashon/ damas Makawaya (dk.13), Samuel Kamuntu, Iddi Mbaga/ Najim Magulu (dk.46), Jabir Aziz.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video