MKALI wa mabao wa Chelsea, Diego Costa amesema ataendelea na 'staili' yake ya kucheza kwa kutumia nguvu kwani ndio imemfanya awe miongoni mwa washambuliaji wanaoogopwa zaidi barani ulaya, lakini amekiri kuwa adhabu ya kufungiwa mechi bado inamsumbua akilini mwake.
Costa amekubaliana na Jose Mourinho ambaye amedai kuwa mfungaji wake huyo anayeongoza orodha ya wafungaji Chelsea akitikisa nyavu mara 17 amepungua kasi yake kutokana na adhabu ya kufungiwa mechi tatu aliyokuwa akiitumikia.
Costa akimkanya makusudi Emre Can wa Liverpool
Nyota huyo rais wa Hispania alifungiwa mechi hizo na chama cha soka England, FA kwa kosa la kumkanyaga Can wa Liverpool.
Costa hajafunga goli lolote tangu katikati mwa mwezi januari na sasa anajiandaa kucheza kwa mara ya kwanza tangu afungiwe siku ya jumapili katika mechi ya fainali ya kombe la Ligi dhidi ya Tottenham uwanja wa Wembley mjini London
0 comments:
Post a Comment