Thomas Ulimwengu wa Taifa Stars (kushoto) akichuana na beki wa Zimbabwe walipokutana mwaka jana uwanja wa Taifa Dar es salaam
TIMU ya taifa ya Tanzania, Taifa stars imepangwa kwenye kundi A katika michuano ya kombe la COSAFA yanayotarajia kufanyika nchini Afrika kusini mwezi mei mwaka huu.
Taifa stars wamepangwa sambamba na Zimbabwe, Lesotho na Namibia katika michuano hiyo ambayo Taifa stars imealikwa kushiriki pamoja na Ghana.
Makundi ya michuano hiyo inayoshirikisha timu za taifa za kusini mwa Afrika yamepangwa usiku wa jana ambapo yamewekwa katika makundi mawili.
Vinara wa kila kundi wataingia hatua ya robo fainali ambapo watajumuika na timu nyingine sita ambazo ni Malawi, Zambia, Afrika kusini, Botswana, Ghana na Msumbiji.
KUNDI A
A1 - Namibia
A2 - Lesotho
A3 - Zimbabwe
A4 - Tanzania
A1 - Namibia
A2 - Lesotho
A3 - Zimbabwe
A4 - Tanzania
KUNDI B
B1 - Seychelles
B2 - Madagascar
B3 - Mauritius
B4 - Swaziland
B1 - Seychelles
B2 - Madagascar
B3 - Mauritius
B4 - Swaziland
0 comments:
Post a Comment