CHELSEA, TOTTENHAM KAZI IPO KESHO WEMBLEY, COSTA, KANE NANI KUIBUKA KIDUME? CHELSEA wanakabiliana na Tottenham katika mechi ya fainali ya kombe la ligi 'Capital One Cup' kesho usiku uwanja wa Wembley, mjini London. Eden Hazard ni silaha kubwa kwa Chelsea katika mechi ya leo, tutaona namna Kyle Walker atakavyomzuia asishambulie kutokea pembeni. Eric Dier atahitaji kufanya kazi ya ziada kumzua mfungaji bora wa Chelsea, Diego Costa ambaye anatokeo katika kifungo cha mechi tatu. Pia tunatarajia kuona Ryan Mason akipambana kumzuia Cesc Fabregas kumzuia asicheze anavyotaka kutokea eneo la kiungo. Wakati huo kimbembe kingine ni baina ya Gary Cahil na Harry Kane, mshambuliaji hatari wa Spurs. Tusubiri kuona nani ataibuka kidume na kubeba kombe la kwanza msimu huu.
0 comments:
Post a Comment