Thursday, February 26, 2015


NAHODHA wa zamani wa timu ya taifa ya Italia Fabio Cannavaro amehukumiwa kufungwa jela miezi 10 kwa kosa la kuvunja sheria baada ya kushindwa kuvikomboa vitu vyake vilivyokamatwa na mamlaka ya mapato nchini Italia.
Cannavaro ,41, ambaye kwa sasa ni kocha wa klabu ya Guangzhou Evergrande Taobao ya nchini China amekuwa akifanyiwa uchunguzi kwa muda mrefu juu ya ukwepaji wa kulipa kodi na Oktoba mwaka jana mamlaka ya kodi huko mjini Naples ilikamata  baadhi ya vitu vyake na mkewe vyenye thamani ya Euro milioni 1 .
Hivyo baada ya kushindwa kwenda kuvikomboa vitu hivyo mahakama nchini humo imetangaza hukumu ya miezi 10 kwa mchezaji huyo wa zamani wa Real Madrid,huku mke wake Daniela Arenoso  akifungwa miezi 4 na mdogo wa mchezaji huyo Paulo Cannavaro anayechezea klabu Sassuolo akifungwa miezi 6 jela.
Hata hivyo watatu hao wamekata rufaa juu ya hukumu hiyo hivyo wanasubiria mpaka mahakama ikutane tena kwa ajili ya kutoa maamuzi ya mwisho juu yao.
Aidha mamlaka ya mapato nchini Italia imeripoti kuwa kampuni ya mchezaji huyo inayoitwa FD Service inadaiwa kodi ya Euro milioni 1 ambayo haikulipwa kati ya mwaka 2005 na 2010.
Cannavaro ambaye alivichezea vilabu vya Parma,Internazionale,Juventus na Real Madrid alishinda tuzo ya Ballon D'or mwaka 2006 baada ya kuiongoza timu ya taifa ya Italia kutwaa kombe la dunia mwaka huo nchini Ujerumani.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video