Na Richard Bakana, Dar es salaam
NAHODHA wa klabu ya Yanga SC na Timu ya Taifa ya Tanzania , Nadir Haroub ‘Cannavaro’ ametoboa siri ya kufanya kwake vizuri katika mchezo wa Soka ni Muziki wa Bongo Flaver.
Cannavaro ambaye kwa sasa yupo nchini Botswana kujiandaa na mchezo wa kimataifa wa marudiano kwenye kombe la Shirikisho barani Afrika, Dhidi ya BDF XI utakopigwa kesho ijumaa, amesema anaposikiliza muziki wa kizazi kipya huwa anapata morali ya kufanya kazi kwa nguvu na kujituma zaidi Uwanjani.
“Nikiwa safarini huwa napenda sana kusikiliza Bongo fleva, Kwa upande mwingine nikishasikiliza Bongo fleva huwa Napata morali ya kucheza sana mpira” Amesema Cannavaro.
Mchezaji huyo ambaye kwasasa ni roho ya Yanga katika safu ya ulinzi amesema kuna wasanii wa Tanzania ambao huwa anapenda kusikiliza kazi zao kila zinapotoka pamoja na zile nyimbo ambazo zinafanya vizuri katika soko la muziki nchini.
“Kuna wasanii wengi tu wananivutia, lakini mimi huwa napenda sana kumsikiliza Diamond, Ali Kiba, Kassim Mganga, Mwana FA, Charles Baba wengi sana lakini mimi huwa napenda sana kusikiliza Bongo Fleva” Amesema Nadir Haroub ‘Cannavaro.
0 comments:
Post a Comment