Wachezaji wa Ghana wakishangilia ushindi wao mbele ya kocha Avram Grant
NDOTO za Equatorial Guinea kutwaa ubingwa wa kombe la mataifa ya Africa, Afcon 2015 baada ya kufungwa mabao 3-0 na Ghana, lakini aibu kubwa imetawala baada ya mashabiki wa timu mwenyeji kufanya vurugu kubwa katika uwanja wa Malabo jana usiku na kusababisha mechi kusimama kwa dakika 35.
Wenyeji wameonesha kiwango kikubwa na maajabu makubwa katika michuano ya mwaka huu, lakini kutolewa hatua ya nusu fainali kuliwaudhi mashabiki ambao walirusha chupa kwa wachezaji wa Ghana, viongozi na mashabiki.
Wachezaji wakisubiri Helkopta iwatulize mashabiki ili mechi iendelee
Mashabiki wakificha nyuso zao wakati Helkopta inapita juu yao
Polisi wakipiga mabomu ya machozi kuwatawanya mashabiki waliokuwa wanafanya vurugu uwanja wa Malabo
Wachezaji wa Ghana wakitolewa chini ya ulinzi mkali
Shabiki wa Guinea ya Ikweta akiwa ametiwa mbaroni
Chupa za maji zikiwa zimesamba katika uwanja wa Malabo
0 comments:
Post a Comment