Kocha wa klabu ya Liverpool Brendan
Rodgers amemfananisha kiungo mshambuliaji wa klabu hiyo raia wa Brazil Philippe
Coutinho na mshambuliaji aliyetimkia katika klabu ya fc Barcelona Luis Suarez
baada ya mchezaji huyo kuonyesha kiwango cha juu katika siku za hivi karibuni.
Goli la dakika za mwisho la mchezaji
huyo ambae alionyesha juhudi binafsi na kufunga goli hilo na kuipeleka klabu ya
Liverpool raundi ya tano lilimzolea sifa kemkem na kocha wake kumfananisha na
Luis Suarez.
Brendan Rodgers alisema Coutinho
ameongeza kiwango katika uchezaji wake siku za hivi karibuni na anastaili
pongezi kwani ameisaidia klabu kwa kiasi kikubwa sana.
“Ni mchezaji ambae anaongeza kiwango
kila kukicha kwa kasi ya ajabu na amefanikiwa kwa kiasi kikubwa uisaidia klabu
kuweza kuibuka na ushindi katika mechi za hivi siku za karibuni licha ya kupata
changamoto za hapa na pale.
0 comments:
Post a Comment