MABINGWA mara 24 wa ligi kuu Tanzania bara, Dar Young Africans watachuana na Platinum ya Zimbabwe raundi ya kwanza ya kombe la shirikisho barani Afrika.
Platinum wameilaza mabao 2-1 Sofapaka ya Kenya katika mechi ya marudiano iliyopigwa jioni ya leo, mjini Harare.
Mechi ya kwanza wiki mbili ziliopita, Platinum waliitandika Sofapaka 2-1, hivyo wanafuzu kwa wastani wa mabao 4-2.
Yanga jana walichapwa 2-1 na BDF XI ya Botswana, lakini walifuzu kwenda raundi ya kwanza kwa wastani wa mabao 3-2 kutokana na ushindi wa 2-0 waliopata uwanja wa Taifa, Dar es salaam majuma mawili yaliyopita.
Yanga dhidi ya Platinum ndio biashara ijayo kwa Watanzania.
0 comments:
Post a Comment