Saturday, February 28, 2015

MABINGWA watetezi wa ligi kuu soka Zanzibar, KMKM wametupwa nje ya michuano ya ligi ya mabingwa Afrika baada ya kushinda goli 1-0 dhidi ya Al Hilal ya Sudan.
Goli hilo pekee katika mechi ya marudiano iliyopigwa uwanja wa Amaan Zanzibar limefungwa Faki Mwalimu.
Mechi ya kwanza nchini Sudan, Al Hilal walishinda 2-0, hivyo walihitaji kutoa sare ya aina yoyote au kutofungwa zaidi ya goli 1-0.
Kwa matokeo ya leo, KMKM wametolewa kwa wastani wa mabao 2-1.
Usiku huu Azam fc wanajitupa uwanjani kuchuana na Al Merrick ya Sudan katika mechi ya marudiano ya ligi ya Mabingwa Afrika inayopigwa mjini Khartoum Sudan.
Mechi ya kwanza Azam walishinda 2-0 uwanja wa Azam Complex na leo wanahitaji sare ya aina yoyote ile au kutofungwa zaidi ya goli moja.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video