Friday, February 6, 2015


Kiungo wa klabu ya chelsea anaecheza kwa mkopo katika klabu ya Everton ambaye kwa sasa anaitumikia timu yake ya Taifa ya Ghana Christian Atsu, amesema anaamini timu ya Ghana itaigalagaza Ivory Coast katika mchezo wa fainali kombe la Mataifa Barani Afrika siku ya Jumapili.

Ghana ilifuzu hatua hiyo baada ya kuwafunga wenyeji timu ya Taifa ya Equatorial Guinea kwa mabao matatu kwa bila, na kuzua taaruki kwa upande wa mashabiki kitu kilicholazimisha mchezo huo kusimamishwa kwa takribani nusu saa.
Magoli ya mapacha Jordan na Andre Ayew pamoja na Mubarak Wakaso ndio yaliyoiwezesha Ghana kufuzu hatua ya fainali na Ivory coast ilifanikiwa kuitoa timu ya taifa ya Algeria katika hatua ya Nusu fainali kwa kuifunga mabao matatu kwa moja.


"Nafahamu Ivory coast ni timu nzuri yenye wachezaji wengi wazuri wanaocheza soka la kulipwa barani ulaya lakini tutafanya kila linalowezekana kuhakikisha tunaifunga katika mchezo wa fainali na kutwaa ubingwa huu wa kombe la mataifa barani afrika mwaka huu,"alisema Atsu

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video