Mshambuliaji nyota wa City Themi Felix amewashukuru mashabiki wa timu yake nchini kote kwa sapoti wanaitoa ndani na nje ya uwanja.
Themi aliye kwenye kiwango bora hivi sasa amesema ameshangazwa na utamaduni wa mashabiki wa City kusafili na timu yao kwa ajili ya kuishaangiliaa popote pale inapokwenda tofauti na ilivyo kwenye timu zingine ambazo hupata nguvu ya mashabiki pindi zinapocheza nyumbani pekee.
“Nawapongeza, nimeshangazwa na hili, tunakuwa pamoja nao popote hata kama ni kwenye michezo ya kirafiki hili ni jambo zuri sana awali nilikuwa naliona kwa vilabu kongwe lakini sasa ni tofauti, mashabiki wa city wameleta kitu kipya kwenye mpira wa nchini yetu, uwepo wao mara zote huwa unatufanya sisi wachezaji kujua kuwa tuna deni kubwa kwao. inatubidi kucheza kwa nguvu na juhudi kubwa ili kuwapatia ushindi kitu ambacho ndiyo malipo pekee kwa kile wanachokifanya, binafsi nawashukuru” alisema.
0 comments:
Post a Comment