Saturday, February 28, 2015

Reina Mgungilia (kushoto) akichuana na Shaaban Kisiga mwaka jana timu hizo zikitoka sare ya 1-1 uwanja wa Taifa

KIUNGO wa ulinzi wa Azam fc anayecheza kwa mkopo katika klabu ya Stand United ya Shinyanga, Reina Mgungila amefanya mahojiano maalumu na mtandao huu na kueleza mambo mbalimbali yanayohusu soka lake na maisha ya kawaida.
Reina alifanya kazi ya kuwaficha viungo wa Simba siku waliposhinda bao 1-0 juma lililopita katika mechi ya ligi kuu uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga.
Nyota huyo kinda anayenyumbuka dimba la kati anajiandaa na mechi ya leo jioni dhidi ya Kagera Sugar uwanja wa Kambarage na mahojiano yamekwenda kama ifuatavyo:

Mwandishi: Siku unayoshinda mechi dhidi ya timu kubwa, mfano Simba Mpenzi wako anakwambia maneno gani?

Reina: Aaaah! kaka! mambo yanakuwa mazuri sana! Ananipa mautamu kweli kweli! Baby wangu ananipigia simu na kuniambia maneno mazuri ya pongezi "Honey nimeona ulivyocheza vizuri, laah! umenikosha sana. Pole kwa mchezo, lakini hongera sana kwa ushindi.

Mwandishi: Mitandao gani ya kijamii unapenda zaidi kutumia na kwanini?

Reina: Napenda sana facebook, watsApp pia naitumia. Facebook inaniunganisha na marafiki wengi, natumia kuwasiliana na timu zilizopo nje, kiukweli facebook inanisaidia sana.
Mwandishi: Nini kinakukera katika soka la Bongo?

Reina: Yapo mengi kaka! lakini kubwa zaidi ni marefa. Wanaboronga sana katika maamuzi, wanaziumiza sana timu hasa za chini. Muda mwingi wanaamua kwa kuangalia huyu ni nani, kama ni mdogo basi wanakunyonga.

Mwandishi: Vipi maisha katika klabu ya Stand United?

Reina: Stand United maisha yanakwenda vizuri. Hii ni timu nzuri japokuwa ni changa ligi kuu. Ina vijana wanaojua kupambana katika hali zote. Namimi nimekuwa tegemezi kubwa kwa Stand.

Mwandishi: Vipi matumaini yako kuelekea mechi ya leo jioni dhidi ya Kagera Sugar?

Reina: Kwakweli leo ni ushindi, wachezaji tumejiandaa vizuri, tumezingatia maelekezo ya kocha, tuna afya nzuri. Kila mtu yupo freshi kiroho safi.

Mwandishi: Vipi mpango wako wa baadaye?

Reina: Kwanza najituma ili nirudi nyumbani, CV zimeshaenda, mabosi wanaiona kazi yangu. Kuna timu zinanimendea, lakini Azam ndio nyumbani, nikimaliza msimu nataka kurudi.
Reina Mgungila

Mwandishi: Timu gani umewahi kucheza kabla ya kujiunga na Azam fc?

Reina: Nilicheza Super Red ya Yombo Vituka 2005, niliitumikia River Irose ya Banana mwaka 2007, mwaka 2008 nikaenda Vijana Benjamini ya Ilala. Nakumbuka 2009 niliitumikia Friends Rangers ya Magomeni na 2011 nikatua Azam fc ya Chamazi Dar es salaam.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video