Mchezo wa ligi kuu ya vodacom Tanzania Bara kati ya Mbeya City Fc na Polisi Morogoro uliochezwa kwenye uwanja wa Jamhuri juzi umemalizika kwa wenyenji kuibuka na ushindi wa bao 1-0.
Polisi walipata bao hilo kipindi cha pili kufuatia mpira mrefu ulipigwa kutoka katikati ya uwanja na baadae kuunganishwa na Said Bahanuzi baada ya mlinzi Yusuph Abdalah kushidwa kuuokoa.
Mara baada ya mchezo huo, kocha Juma Mwambusi aliwataka vijana wake kutokukata tamaa kwa matokeo haya na kuahidi kujiandaa vizuri ili kupata matokeo kwenye mchezo unaofuata mwishoni mwa juma lijalo dhidi ya JKT Ruvu kwenye uwanja wa Chamanzi Complex jijini Dar es Salaam.
“Tumepoteza mchezo, lakini tusikate tamaa, tuna mchezo jumamosi ijayo ni vyema tuelekeze nguvu huko alisema Mwambusi.
0 comments:
Post a Comment