MAKAMU wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange Kaburu ameendelea kukanusha taarifa za yeye kusimamishwa kwenda kwenye kambi ya klabu hiyo ndani na nje ya Dar es Salaam.
Baadhi ya wanachama wa Simba walimshutumu Kaburu kuwagawa wachezaji, kumpangia kocha kikosi, hivyo wakapendekeza asiende kambini na aache mara moja tabia hiyo.
Kaburu alikanusa shutuma hizo na kuahidi kuwashukulia hatua hususani mwenyeketi wa tawi la Mpira Pesa, Magomeni, Ustadh Masoud ambaye alisema wazi wazi kuhusu Kaburu kumpangia kocha kikosi.
Makamu huyo wa Rais amekaririwa na kituo kimoja cha redio jijini akisema kuwa yeye kutokwenda kambini ni mgawanyo wa madaraka tu.
"Kuna kamati mbalimbali zinafanya kazi, mimi naenda kambini kama kuna jambo la muhimu, kuhusu kuzuiliwa sio kweli". Amesema Kaburu.
Hata hivyo siku za karibuni Kaburu hajaonekana katika kambi ya Simba mjini Morogoro na Shinyanga kitu ambacho hakikuzoeleka.
Mechi ya Shinyanga Simba wakifungwa 1-0 na Stand, Vigogo wa Simba walikuwepo akiwemo Rais Evans Aveva na mwenyekiti wa kamati ya usajili, lakini Kaburu hakuwepo.
Kaburu alizoeleka kuonekana kambini kwa Simba na kwenye mazoezi ya klabu hiyo, lakini kwasasa haonekani.
"Nina mawasiliano mazuri na bosi wangu, Rais wa klabu, tunaendelea kufanya kazi pamoja".
"Inawezekana kuwa baadhi ya viongozi wanajaribu kupenyeza maneno ya chuki au maneno ambayo hayawezi kuleta umoja ndani ya klabu ya Simba.
"Wanasimba wana uelewa, sisi viongozi tunatengeneza timu mpya, mwalimu ni mpya, tunachopitia sahizi ni changamoto za mpira. Timu ni ya vijana wenye vipaji wasiokuwa na uzoefu, tuwape muda. Tukishaanza kupata matokeo, haya yote tutayasahau.
0 comments:
Post a Comment