YANGA yenye kumbukumbu ya ushindi wa goli 1-0
iliovuna mwishoni mwa wiki iliyopita Uwanja wa Jamhuri Morogoro dhidi ya Polisi
Moro inawania pointi tatu zingine jumapili, februari 1 mwaka huu itakapocheza
na Ndanda fc uwanja wa Taifa Dar es salaam.
Hiyo itakuwa mechi ya nne ya ligi kuu kwa kocha
Hans Van Pluijm ambaye alianza kwa sare ya mabao 2-2 na Azam fc Desemba 28
mwaka jana akirithi mikoba ya Mbrazil, Marcio Maximo.
Baadaye akatoka suluhu (0-0) na Ruvu Shootings,
Januari 17 mwaka huu. Mwishoni mwa wili iliyopita alishinda 1-0 dhidi ya Polisi
Moro.
Katika mechi tatu alizocheza na kushinda moja,
Pluijm ameonekana kufanikiwa kuijenga Yanga inayocheza mpira wa pasi na
kushambulia kwa kasi tofauti na kipindi cha Marcio Maximo ambapo Yanga walikuwa
wanajihami sana.
Hata hivyo, bado kikosi hicho kilichosheheni nyota
wengi akiwemo Mliberia Kpah Sherman, Mrundi Amissi Tambwe, Wanyarwanda Mbuyu
Twite na Haruna Niyonzima, Wazawa Danny Mrwanda, Saimon Msuva kina mapungufu ya
kucheka na nyavu.
Yanga wanatengeneza nafasi nyingi, lakini
umaliziaji ni mbovu na ilifikia hatua uongozi ukaruhusu baadhi ya wanachama
wake kuomba dua la kuondoa nuksi klabuni hapo.
Mbali na mechi hiyo ya jumapili, kesho Jumamosi
kuna mechi nyingine zitapigwa.
Simba watawakaribisha JKT Ruvu uwanja wa Taifa,
Coastal Union watachuana na Mtibwa Sugar uwanja wa Mkwakwani Tanga.
Ruvu Shootings wataikaribisha Stand United uwanja
wa Mabatini, wakati Tanzania Prisons watakuwa nyumbani uwanja wa Sokoine
kuchuana na Kagera Sugar.
Polisi Moro watakabiliana na wababe wa Simba,
Mbeya City fc.
Mechi ya Mgambo na Azam fc haitakuwepo kwasababu
mabingwa watetezi hawapo nchini kwasasa.
Azam fc ipo nchini DR Congo kushiriki mashindano ya
Mazembe yanayoendelea mjini Lubumbashi ikiwa ni maandalizi ya mechi ya ligi ya
mabingwa itakayopigwa mwezi ujao dhidi ya El Merreick ya Sudan.
0 comments:
Post a Comment