Tuesday, January 20, 2015


Na Bertha Lumala, Dar es Salaam 
Uongozi wa Yanga SC umeamua kuvunja ukimya kuhusu kitendo cha baadhi ya wachezaji wa Ruvu Shooting kumchezea undava straika Amisi Tambwe katika mechi yao iliyopita.

Mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu uliopita, Mrundi Amisi Tambwe ameoneshwa katika picha na baadhi ya magazeti nchini akifanyiwa vitendo vya ovyo uwanjani na baadhi ya nyota wa Ruvu Shooting katika mechi hiyo iliyomalizika kwa suluhu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Jumamosi.

Katika kile kilichoonekana kama kukamia mechi, picha za baadhi ya vyombo vya habari vimeonesha Tambwe akifanyiwa vitendo vibaya ndani ya uwanja na baadhi ya wachezaji wa Ruvu Shooting.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga SC, Jerry Muro amesema kesho watazungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuweka wazi kuhusu hatua ambazo wamepanga kuzichukua dhidi ya Ruvu Shooting kutokana na matukio hayo ya kindava kwa Tambwe.

"Amisi Tambwe alidhalilishwa, mimi nitamke wazi, tunakaa kikao kizito ili tuliangalie kwa undani suala hilo. Watu wanasema mpira si lelemama lakini alichofanyiwa Amisi Tambwe ni udhalilishaji, 'football is the fair game' (mpira wa miguu ni mchezo wa kiungwana). 

"Mchezaji wetu amepigwa roba, amepasuliwa mdomo. Kesho tutazungumza na vyombo vya habari juu ya hatua tunazozichukua kutokana na vitendo hivyo.

"Kitendo alichofanyiwa Tambwe si kizuri, tukishatatua hili itajulikana kama atakwenda moro au la. Wapinzani wetu ni wanajeshi lakini askari mwenye weledi hawezi kufanya vitendo hivyo," amesema zaidi Muro.

Tambwe aliyefunga mabao 19 katika mechi 23 alizopangwa kati ya 26 za VPL akiwa na Simba SC msimu uliopita, amefunga mabao mawili tu katika mechi nane alizopangwa kati ya tisa za VPL msimu huu.

Goli moja alilifunga katika sare ya 2-2 ya Simba SC dhidi ya Coastal Union FC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Septemba 21, mwakla jana na katika sare ya 2-2 ya Yanga SC dhidi ya Azam FC Uwanja wa Taifa Desemba 28 mwaka jana.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video