Tuesday, January 6, 2015


SAM_4363
Na Bertha Lumala
Mabingwa mara 24 wa Tanzania Bara, Yanga SC wameng'ara katika Kundi A baada ya kuifunga bao 1-0 timu kibonde ya Shaba FC ya Pemba katika mechi yao ya mwisho ya kundi hilo ambayo imechezwa Uwanja wa Amaan, Zanzibar usiku huu.

Bao la 'usiku' la dakika ya 86 la kiungo mshambuliaji Andrey Coutinho limeiokoa Yanga SC kutoka kwa aibu Uwanja wa Amaan kwani timu hiyo ilikuwa imefungwa na timu nyingine zote za Kundi A, Taifa ya Jang'ombe na Polisi Zanzibar.

Coutinho aliitendea haki krosi murua ya beki wa pembeni Juma Abdul kutoka wingi ya kulia Kaskazini mwa Uwanja wa Amaan.

Nyota wa Yanga SC, Mrisho Ngasa, Danny Mrwanda, Simon Msuva, Amisi Tambwe na Coutinho walikosa mabao mengi katika vipindi vyote kiasi cha kuwashawishi baadhi ya mashabiki wa Jangwani kuamini kulikuwa na 'kitu' langoni.

Maajabu zaidi yalioneshwa katika robo tatu ya saa ya mchezo mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), Tambwe kupaisha akiwa mita tatu kutoka mstari wa goli la Shaba FC.

IMANI ZA KISHIRIKINA
Licha ya ukubwa wa jina lao, Yanga FC waelazimika kuuweka pembeni weledi wao na kuonesha imani za kishirikina baada ya shabiki wa timu hiyo kutoka Dar es Salaam 'Carros' kuvamia uwanjani na kuzichukua glovu za kipa Bakari Shawaji wa Shaba FC akiamini zilikuwa na 'uchawi' ndiyo maana nyota wao wakakosa mabao.

Hata hivyo, shabiki huyo alijikuta akiishia mikononi mwa polisi na kupelekwa 'central' kwa kufanya vurugu uwanjani.

Walioanza Yanga SC: Deogratius Munishi, Juma Abdul, Edward Charles, Zahir Rajabu, Kelvin Yondani,

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video