Tuesday, January 20, 2015


Na Bertha Lumala, Dar es Salaam 
Licha ya kuajiri watendaji wapya wenye weledi, Yanga SC imekubaliana na wazo la baadhi ya wanachama wake kusomwa dua maalum kuondoa nuksi katika kikosi chao.

Hivi karibuni Yanga SC ilitangaza kuwatimua baadhi ya watendaji wake na kuajiri wataalam wapya wakiwamo mtangazaji wa zamani wa ITV na TBC, Jerry Muro ambaye pia aliibuka mwandishi bora wa habari wa mwaka pamoja na Daktari wa Michezo, Jonas Tiboroha.

Lakini, Yanga SC leo imeamua kusahau weledi wa watendaji wake wapya na kuridhia wazo la kusomwa kwa dua ili "kuondoa mikosi kwenye kikosi cha Jangwani."

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga SC, Muro amesikika katika Kipindi cha 'Spoti Leo' cha Radio One Stereo usiku huu akisema: "Hawana kizuizi na wanachama wao wanaotaka isomwe dua kuondoa mikosi kikosini."

Ikumbukwe kuwa Yanga SC licha ya kuwa na wachezaji wakali wakiwamo watano wa kimataifa, Warwanda Haruna Niyonzima na Mbuyu Twite, Mliberia Kpah Sherman, Mbrazil Andrey Coutinho na Mrundi Amisi Tambwe imeshindwa kung'ara katika michuano ya Kombe la Mapinduzi ikifungwa 1-0 na JKU na haina matokeo mazuri katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) ikiwa nafasi ya nne baada ya kubanwa na Ruvu Shooting Jumamosi.

"Watu wanasema sisi tumeingia wa kisasa, lakini Bakiri Makele (Mwenyekiti wa Vijana wa Yanga SC) na wenzake wanasema na wamelifanyia ufafanuzi MZURI suala hilo. Timu hii ni ya wanachama, si ya Jerry Muro na Tiboroha. 

"Tuko tayari jambo lolote lifanyike klabuni mradi liwe na maslahi ya timu na ustawi wa klabu. Kuna tofauti ya kutambika na kusoma dua. Sisi tunataka kusoma dua na si kutambika. Makele ameeleza vizuri kuhusu suala hili," amesema Muro. 

Katika hatua nyingine, Muro amesema timu yao leo asubuhi imefanya mazoezi mepesi Uwanja wa Kawe na itaingia kambini kesho Bagamoyo na keshokutwa majira ya mchana wataanza safari kwenda Morogoro, tayari kumenyana na maafande wa Polisi Moro Uwanja wa Jamhuri mjini humo Jumamosi.

Kuhusu afya ya mchezaji kiraka Mbuyu Twite, Muro amesema Mrwanda huyo mwenye asili ya DRC ameimarika kiafya na kuna uwezekano mkubwa wa kwenda naye Mji Kasoro Bahari.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video