Friday, January 9, 2015


DSC03160
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro
Na Bertha Lumala
Wakati uongozi wa mabingwa mara 24 wa Tanzania Bara, Yanga SC umetangaza rasmi kumtema kipa mzoefu Juma Kaseja baada ya kuvunjwa kwa mkataba wake, imefahamika kuwa kipa huyo muda wowote atafunguliwa mashtaka katika vyombo vya soka akitakiwa kulipa fidia ya Sh. milioni 340.

Jana Jumatato, uongozi wa Yanga SC uliokuwa Zanzibar, ulitangaza rasmi kuachana na kipa huyo ikiwa ni siku chache baada ya Desemba 31, mwaja jana kuwasilisha orodha ya wachezaji 24 katika Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) kwa ajili ya michuano ya mwaka huu ya Kombe la Shirikisho bila jina la Kaseja.

Majina ya makipa watatu wa Yanga SC yaliyowasilishwa CAF ni; Deogratius Munishi 'Dida', Ali Mustafa 'Barthez' na Alphonce Majogo aliyesajiliwa dirisha dogo akitokea Friends Rangers ya Dar es Salaam inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara (FDL).

Mtandao huu umepata taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Yanga SC zikieleza kuwa mbali na kuachana na kutangaza kumtema rasmi Kaseja, kipa huyo atafunguliwa mashtaka ili alipe Sh. milioni 340 ikiwa ni kuridisha fedha ya usajili Sh. milioni 40 baada ya kukiuka masharti ya mkataba na Sh. milioni 300 ambayo ni fidia kwa klabu kwa kukosa huduma yake kwa kukacha kambi ya Yanga SC bila taarifa.

SAKATA LILIVYO
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye Hoteli ya Zanzibar Ocean View mjini Unguja jana mchana, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga SC, Jerry Muro alisema klabu hiyo imeamua kuachana na kipa huyo chaguo la kwanza la zamani la Taifa Stars kutokana na kukiukwa kwa masharti ya mkataba kati ya pande hizo mbili.

Muro alisema kuwa Novemba 8, 2013, usajili wa miaka miwili wa Kaseja Yanga ulifanyika akipewa Sh. milioni 20 za utangulizi kati ya Sh. milioni 40 za ada ya kusaini mkataba kuitumikia klabu hiyo ya Jangwani.

Aliendelea kufafanua kuwa Januari Mosi, 2014 Yanga ilimlipa Kaseja Sh. milioni 20 alizokuwa akiidai ikiwa ni ada ya usajili.

Hata hivyo, Muro alisema Kaseja aliwasilisha barua Yanga Novemba 11, 2014 akilalamika kutopangwa mara nyingi kwenye kikosi hicho cha wanajangwani huku pia akitaka kukatiwa bima.

"Desemba 12, 2014 Yanga ilimjibu Kaseja kwamba taratibu zote anazijua kuhusu masuala ya bima za matatizo makubwa ya wachezaji 'serious injuries' na kumkumbusha kuwa suala la kupangwa kikosini liko chini ya benchi la ufundi. 

"Isitoshe Kaseja alipangwa katika mechi nyingi za Yanga, alicheza dhidi ya Mtibwa Sugar, CDA ya Dodoma na timu moja ya Shinyanga. Katika michezo tunajua mchezaji hawezi kuwa 'fiti' wakati wote.

"Desemba 31, 2014 akaleta barua nyingine akidai suala la bima na kutopangwa katika mechi nyingi. Tukaona Juma Kaseja hana hoja za msingi, kama imeshalipwa, kwa nini aendelee kuwa hivyo? Tukaona hapa kuna kitu.

"Msimamo wa klabu tunamwacha aende zake. Usipoonekana katika kambi na mazoezi ya timu yetu kwa siku mbili bila kutoa taarifa, kwa mujibu wa mikataba ya Yanga na wachezaji, unakuwa umevunja mkataba.

"Kama yeye alimwaga mboga, na sisi (Yanga) tunamwaga ugali," alisema zaidi Muro aliyekuwa amefuatana na kocha mkuu Mholanzi Hans van der Pluijm na nahodha Nadir Haroub 'Cannavaro'.

Kaseja aliyelelewa Simba SC, alijiunga na Yanga SC katika misimu miwili tofauti lakini ameshindana na wanajangwani huku pia akitemwa katika kikosi cha Taifa Stars.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video