Friday, January 9, 2015


???????????????????????????????
Na Bertha Lumala
KAMATI ya mashindano ya Kombe la Mapinduzi mwaka huu, imewashukuru mashabiki, klabu, taasisi na watu wote waliofanikisha na wanaoendelea kusaidia kufanikiwa kwa michuano hiyo mwaka huu huku ikiweka wazi kwamba Yanga SC ndiyo timu iliyokuwa ikiingiza watu wengi zaidi uwanjani.

Katibu wa kamati hiyo, Hamis Abdallah Said amekutana na waandishi wa habari kwenye moja ya Kumbi za Uwanja wa Amaan visiwani Zanzibar leo alasiri na kufafanua mambo mbalimbali kuhusu mashindano hayo yanayofanyika kwa mara ya tisa mwaka huu kuenzi Mapinduzi Tukufu ya Zanzibar yaliyofanyika Januari 12, 1964.

Katibu huyo ameanza kwa kufafanua namna mashindano hayo yanavyoendesha kwa kuhusisha taasisi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Shirika la Umeme Zanzibar, vyombo vya habari, Chama cha Soka Zanzibar, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Azam Marine ambao wamesafrisha timu zote kuja hapa Zenj na watu mbalimbali waliofanikisha kufanyika kwa mashindano hayo.

 
"Kwa ujumla mashindano yamekwenda vizuri. Mechi zote zimekwenda kama zilizopangwa, hapakuwa na matukio makubwa yanayohatarisha amani," amesema.

"Kombe la Mapinduzi ni kama fainali za Kombe la Dunia hapa Zanzibar. Idadi kubwa ya wananchi kutoka Zanzibar na Tanzania Bara pamoja na vyombo vya habari kutoka mataifa ya nje vimepiga kambi hapa kwa ajili ya michuano hii.

"Tumeridhika na hali ya uamuzi ingawa kulikuwa na matatizo kidogo ya kibinadamu na pengine yapo ya makusudi lakini hatujui zaidi kuhusu hilo.

"Pengine hofu pia kwa marefa wetu kutokana na ukubwa wa mashindano haya na timu zinazoshiriki.

Kulikuwa na tatizo la ushirikina pia katika baadhi ya mechi ikiwa ni pamoja na mechi ya mwisho ya Kundi A kati ya Yanga  na Shaba FC. Kamati haiamini katikia imani hizo na inazishauri klabu kuachana na vitendo hivyo. Wajiandae kikamilifu kimazoezi, huu ndiyo msimamo wa kamati katika hilo. Hatuamini katika ushirikina," kiongozi huyo amesema zaidi.

Amesema wamesikia malalmiko ya JKU kwamba ndani ya vyumba vyao vya jkubadilishia nguo wakati wa mechi yao dhidi ya Yanga vilikuwa vimemwagwa dawa za kienyeji kwa imani za kishirikina, lakini hawajapata malamiko hayo rasmi.
Kamati pia imewaomba radhi mashabiki kutokana na tatizo la foleni katika kuingia uwanjani lililojitokeza wakati wa mechi ya Yanga dhidi ya JKU huku ikiahidi kulifanyia marekebisho katika mechi zijazo.

ZAWADI
Kamati pia imekumbusha kuwa itatoa zawadi ya Sh. milioni 10 kwa bingwa na Sh. milioni tano kwa mwanafainali atayeshindwa.

Aidha, kamati pia imetangaza kuwa itatoa zawadi ya ving'amuzi kwa mchezaji bora, kipa bora na mfungaji bora wa michuano hiyo mwaka huu, zawadi hiyo ikitolewa na Azam Tv.

MAPATO SH. MILIONI 117
Katika hatua nyingine, kamati imetangaza kuwa katika mechi zote zilizopita, imepata Sh. 116,798,500 kutokana na viingilio huku mechi zilizozihusisha klabu kongwe nchini, Simba na Yanga zikiingiza kiasi kikubwa zaidi ya fedha na mashabiki.

"Tunawashukuru Simba, Yanga, Azam na Mtibwa kwa kukubali kuja hapa kushiriki. Mechi za Yanga zilikuwa na mapato makubwa zaidi kuliko timu nyingine wakifuatiwa na Simba.

"Kamati imetumia Sh. 83,364,000. hivyo tunayo 'balance' (ziada) ya Sh. milioni 33 hivi. Kwa maana hiyo tunao uwezo wa kutoa zawadi na hatutakuwa ba deni kama ilivyokuwa mwaka jana," amesema.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video