Monday, January 5, 2015

8 (1)
Hatua ya makundi ya michuano ya Kombe la Mapinduzi mwaka huu itafungwa kesho kwa mechi nne za Kundi A na B Yanga wakichuana na Shaba FC ya Pemba Uwanja wa Amaan, Zanzibar saa 2:15 usiku.
Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema kuwa anaamini kikosi chake kitaendelea kupata ushindi mnono kutokana na kupangwa na timu vibonde katika Kundi A la michuano hiyo inayofanyika kwa mara ya tisa.
11
Mbali na Shaba FC, Yanga SC imepangwa na wawakilishi wa Zanzibar katika michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika mwaka huu, Polisi FC pamoja na Taifa ya Jang’ombe inayoshiriki Ligi Daraja la Pili Zanzibar, timu ambazo zimepokea vichapo vya mabao 4-0 kila moja kutoka kwa Yanga.
“Timu za Zanzibar ni nzuri lakini haziko katika ligi iliyo bora. Ninaamini tutashinda mechi zote za hatua hii ya makundi kwa sababu hatuna wapinzani wa kweli. Ni ukweli kwamba soka la Zanzibar liko chini,” amesema raia huyo wa Uholanzi.
Mechi nyingine ya mwisho ya Kundi A itazikutanisha Polisi na Taifa ya Jang’ombe Uwanja wa Mao Tse Tung visiwani hapa saa tisa alasiri. Timu hizo zote zina pointi tatu zilizozivuna baada ya kuifunga bao 1-0 Shaba FC.
Mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), Azam FC watakamilisha hatua hiyo kwa kumenyana na Mtende katika mechi yao ya mwisho ya Kundi B itakayochezwa Uwanja wa Amaan 11 jioni.
Kocha Mkuu wa Azam FC, Mcameroon Joseph Omog amesema itakuwa mechi ngumu kwa sababu baadhi ya timu za Zanzibar zimeimarika. KMKM tuliyocheza nayo jana, si KMKM ya miaka iliyopita.”
Mechi nyingine ya mwisho ya Kundi B inahusisha mabingwa watetezi wa michuano hiyo KCCA FC ya Uganda dhidi ya mabingwa wa Zanzibar KMKM Uwanja wa Amaan kuanzia saa 9:00 alasiri.
“Si kazi rahisi kwetu kutetea ubingwa wa mashindano haya mwaka huu kwa sababu ya ubora wa vikosi vya timu kama Yanga, Mtibwa na Azam, lakini pia baadhi ya timu za hapa Zanzibar.
“KMKM wanacheza vizuri, tutajipanga tuwafunge ili tumalize nafasi ya kwanza katika kundi letu,” amesema Kocha Mkuu wa KCCA FC, Mganda Abdallah Mubiru visiwani hapa leo asubuhi.
Michuano hiyo itaendelea keshokutwa kwea hatua ya Robo-Fainali kinara wa Kundi C atakapovaana na timu itakayomaliza nafasi ya tatu katika hatua ya makundi (best looser 2) ikizidiwa kidogo na timu itakayomaliza nafasi ya tatu katika hatua ya makundi ikiwa na pointi nyingi (best looser 1).
Mechi hiyo itachezwa Uwanja wa Amaan kuanzia saa 10 jioni kabla ya mechi ya pili ya robo-fainali itakayokutanisha timu itakayomaliza nafasi ya pili katika Kundi B dhidi ya timu itakayomaliza nafasi ya pili katika Kundi C.
Alhamisi kutakuwa na mechi mbili za robo-fainali kinara wa Kundi A akipambana dhidi ya ‘best looser 1′ Uwanja wa Amaan saa 2:15 usiku baada ya kinara wa Kundi B kucheza dhidi ya mshindi wa pili wa Kundi A uwanja huo huo.
Bingwa wa michuano hiyo atapewa zawadi ya Sh. milioni 10 wakati mshindi wa pili atapatiwa Sh. milioni tano za Tanzania.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video