Wanandinga wa Yanga wakifanya mazoezi jana uwanja wa Boko Veteran
YANGA SC imesema Ruvu Shootings watakayochuana
nayo katika mchezo wa ligi kuu uwanja wa Taifa Dar es salaam haina uwezo wa
kuifunga na usajili wake unaoishia Mlandizi tu.
Mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa Yanga,
Jerry Muro amesema usajili wa Yanga ni wa mamilioni, wanakwenda mpaka ulaya,
Liberia, Rwanda na Burundi tofauti na Shootings wanaosajili mpaka Chalinze na
Mlandizi.
“Kikosi bora kinaonekana bwana, sisi usajii wetu
ni wa mamililioni, wenzetu usajili wao wa laki tano, wakisajili sana utakuta wamesajili
kutoka Chalinze, utalinganisha na Yanga ambayo inasajili mpaka Ulaya”. Amesema
Muro. “Tunafika Liberia, Burundi, Rwanda, utafananisha na timu inayosajili
mwisho pale Mlandizi tu, mtutendee haki Yanga, Yanga ni timu kubwa”
Muro ameongeza kuwa Ruvu Shootings ni mtoto wao
ambaye wanamlea na historia inawalinda kwani walishampa magoli 7-0.
“Alishapata magoli saba ya kutosha, tunacheza naye
leo, hatuna wasiwasi kabisa, Yanga ni klabu bora na umri tuliokuwa nao hakuna
mtu yeyote pale Ruvu Shootings mwenye umri kama wetu katika ligi”.
“Mkongwe ni mkongwe tu, hatuna wasiwasi, tuna
wachezaji bora, benchi la ufundi bora, tumejipanga vizuri. Tunacheza mpira bora
sio wa lamli moja jumlisha moja lazima iwe mbili, lazima tupate ushindi.” Aliongeza
Muro.
0 comments:
Post a Comment