Friday, January 16, 2015

Hans van der Pluijm (kushoto) na msaidizi wake Charles Boniface Mkwasa waliifunga Ruvu Shootings 7-0 msimu uliopita, je, watafanya nini kesho?

YANGA SC inawakaribisha maafande wa Ruvu Shootings kutoka Pwani katika mechi ya ligi kuu soka Tanzania bara itayopigwa kesho uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Unapozitaja timu hizi mbili, kumbukumbu inayokuja haraka kichwani ni kipigo cha 7-0 walichotoa Yanga msimu uliopita kwa wanajeshi hawa wanaofundishwa na Tom Alex Olaba.

Kipigo hiki kilitolewa na kocha Hans van der Pluijm na sasa amerejea tena na kukutana na Shootings katika mchezo wake wa pili wa ligi kuu msimu huu.

Ikumbukwe kuwa desemba 28 mwaka huu, Yanga walitoka sare ya mabao 2-2 na Azam fc na Pluijm alisema watafanya marekebisho makubwa kabla ya kucheza mechi inayofuata ambayo ndio kesho.

Kipindi cha Marcio Maximo, Yanga ilikuwa inacheza mpira wa kujilinda zaidi na mashabiki hawakufurahishwa na mfumo huo, lakini ujio wa Pluijm umerejesha soka la kushambulia  zaidi.

Mliberia Kpah Sherman hakuwepo msimu uliopita, je, atafanya nini katika mechi yake ya pili ya ligi kuu?

Kocha huyu raia wa Uholanzi anacheza mpira wa wazi, pasi za uhakika na kushambulia zaidi.

Wakiwa kombe la Mapinduzi, Yanga walishinda mabao 4-0 katika mechi mbili dhidi ya Polisi na Taifa ya Jang’ombe, ingawa walifungwa bao 1-0 na JKU katika mechi ya robo fainali na kutupwa nje ya mashindano.

Mbali na kipigo hicho, Yanga walitengeneza nafasi nyingi lakini Amisi Tambwe, Andrey Coutinho, Kpah Sherman, Mrisho Ngasa, Danny Mrwanda na Saimon Msuva walishindwa kuzitumia.

Kutokana na kasi hiyo, Ruvu Shootings wanajiandaa vikali kuhakikisha wanawazuia washambuliaji hatari wa Yanga.


Wapinzani wa Yanga, Ruvu Shootings ya Pwani

Msemaji wa klabu hiyo, Masau Bwire amesema Yanga sio timu ya kuogopwa, wamejipanga kufuta 7-0.
“Wanajiita wazee wa nne nne, sijui wazee wa wiki, tunataka kuwaonesha Watanzania kuwa timu yetu ina vijana wenye vipaji vya hali ya juu, tunalipa zile 7-0”. Alisema Bwire mwenye maneno mengi mithiri ya Chiriku.

Mechi nyingine za kesho ni Kagera Sugar dhidi ya Mbeya City fc uwanja wa CCM Kirumba mwanza. Ndanda fc watakuwa wenyeji wa Simba uwanja wa Nangwanda Sijaona.

Stand United watawakaribisha Azam fc katika uwanja wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga, wakati Mgambo JKT watachuana na Tanzania Prisons.


Jumapili, JKT Ruvu watacheza na Mtibwa Sugar uwanja wa Azam Complex, Chamazi Dar es salaam na Coastal Union watachuana na Polisi Morogoro uwanja wa CCM Mkwakwani Tanga.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video