Tuesday, January 6, 2015

8 (1)
HATUA ya makundi ya kombe la Mapinduzi inatarajia kumalizika leo kwa mechi nne kupigwa viwanja viwili tofauti hapa visiwani Zanzibar.

Mapema majira ya saa 9:00 alasiri katika uwanja wa Amaan, Mabingwa watetezi wa kombe hilo, KCC ya Uganda watachuana vikali na mabingwa wa Zanzibar, KMKM katika mchezo wa mwisho wa kundi B.

Mabingwa watetezi wa Tanzania bara, Azam fc watahitimisha mechi ya kundi B kwa kuchuana na Mtende, uwanja wa Amaan.

Katika dimba la Mao Dze Tung, Taifa ya Jang’ombe itakuwa kibaruani kuhitimisha mechi ya kundi A dhidi ya Polisi.


Yanga wao watacheza mechi ya mwisho ya makundi kwa kukabiliana na Shaba majira ya saa 2:15 usiku.

Yanga wanaingia katika mechi hii wakiwa tayari wameshafuzu hatua ya robo fainali kwani mechi mbili za kwanza dhidi ya Taifa ya Jang'ombe na Polisi, zote walishinda mabao 4-0

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video