Sunday, January 4, 2015

Kikosi cha Yanga kilichoanza leo

YANGA SC imeendeleza wimbi la ushindi katika michuano ya kombe la Mapinduzi inayoendelea visiwani Zanzibar kwenye uwanja wa Amaan baada ya kuitandika mabao.. timu ya Polisi.
Mbrazil Andrey Coutinho alikuwa wa kwanza kuiandikia Yanga bao la kuongoza katika dakika ya 27 ya kipindi cha kwanza na baadaye dakika ya 33 Mliberia Kpha Sherman aliandika kimiani bao la pili akimalizia mpira mzuri aliotengewa kwa njia ya kichwa na Amissi Tambwe.

Katika dakika ya 56 ya kipindi cha pili, Coutinho aliandika bao la tatu kwa mpira wa adhabu ndogo.

Kikosi cha Polisi kilichoanza aleo

Katika day a 80 Saimon Msuva aliandika bao la nne akimalizia pasi nzuri ya Salum Telela.
Hilo ni bao la nne la Msuva katika mechi mbili tu za mashindano ya Mapinduzi 2015.

Huo ni ushindi wa pili kwa Yanga kwani katika mechi ya kwanza iliyopigwa juzi uwanja wa Amaan, vijana hao wa Hans Van der Pluijm waliitandika Taifa ya Jang’ombe mabao 4-0 ambapo Saimon Msuva alipiga mabao matatu ‘hat-trick’  na moja likifungwa na Sherman.

Yanga chini ya Pluijm wamebadilika kiuchezaji ambapo wanashambulia zaidi tofauti na kipindi cha Marcio Maximo aliyekuwa anatumia mbinu za kujihami zaidi.

Mbali na kushambulia, Yanga wanacheza mpira wa kupasiana kwa dakika zote 90 na kupanga mashambulizi ya maana.

Baada ya mechi hii, majira ya saa 2:00 usiku, mabingwa watetezi wa Tanzania bara, Azam fc watachuana vikali na KMKM ya Zanzibar katika uwanja wa Amaan.


Michuano hiyo itaendelea kesho kwa mechi mbili kupigwa uwanja wa Amaan ambapo Mafunzo wataoneshana kazi na Mtibwa Sugar fc majira ya saa 11:00 jioni na usiku saa 2:00, Simba watachuana na JKU.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video