Na Amplifaya Amplifaya
NILICHOJIFUNZA na
kukigundua kuhusu sisi mashabiki wa Tz kiukweli huwa hatuna uvumilivu na
tunapenda mafanikio ya hapo kwa papo. Hatunaga subira.
Tumekuwa tukihukumu
wachezaji wengi hasa wale wanaotoka nje ya nchi kuja nchini kwetu kucheza soka.
Tunataka wakija Leo
wang'ae Leo Leo .Tunasahau kuna vitu
vingi vinaweza kumsababisha mchezaji kushindwa kung'ara ikiwemo kubadilisha
mfumo aliouzoea.
Jinsi anavyocheza, je ni mchezaji gani alikuwa anamchezesha
kwenye timu aliyotoka na wakati huku alipo sasa hakuna mtu wa aina ile.
Pia ugumu wa ligi, hali ya hewa na mengi kama hayo.
Hivyo mchezaji kama huyu anatakiwa kupewa muda
kuzoea mazingira, mfumo pamoja na wachezaji aliowakuta.
Yanga chini ya Maximo, Coutihno na wenzake walionekana
si chochote kutokana na mfumo mgumu wa kocha huyo.
Upande wa Simba nao kuna baadhi ya watu wanamtupia
lawama Danny_Serunkuma
kitu ambacho sio sahihi maana mchezaji mwenyewe hana hata miezi sita kuichezea
Simba.
Ni wachezaji wangapi walikuja TANZANIA tukawaona
magarasa tukawatimua na wakarudi makwao wakapata timu zakuchezea na wakang'ara
na wakaja kutuhukumu pale pale kunako dimba la taifa?
Mpira hapa bongo kwetu unaongozwa na wasanii
watupu.
Huku wataalamu hawa hawa wachache tulionao wakipigwa mawe na kudharauliwa.
0 comments:
Post a Comment