MTANDAO huu umefanya mahojiano maalumu na Nahodha
wa zamani wa Mtibwa Sugar, Taifa Stars na sasa kocha wa Mtibwa, Mecky Mexime
kuhusu chimbuko la ukocha wake na falsafa anayopenda.
Pia ameeleza mambo mbalimbali ya mpira, leo tuanza
sehemu ya kwanza ya mahojiano haya:
Mwandishi:
Chimbuko au historia yako ya kuingia katika kazi ya ukocha ni nini?
Mexime: Kitu
cha kwanza, mimi nimecheza mpira muda mredu, nilikuwa nahodha, ujue kuwa
nahodha nako kunasaidia, unakuwa kama
kiongozi.
Mpaka alipokuja Marcio Maximo akanichagua kuwa
nahodha wake. Alituweka wengi wengi, akawa anachunguza, lakini akaona mimi naweza
kuwa nahodha wake.
Tukafanya naye kazi mwaka wa kwanza, lakini siku moja
Maximo baada ya kufanya naye kazi kwa mwaka mmoja akaniambie wewe ni kiongozi
mzuri, ukimaliza mpira somea ukocha. Utakuja kuwa kocha mzuri.
Ujue alikuwa kama rafiki yangu, kama anataka
mchezaji wa kimataifa ilikuwa ananiomba ushauri, hata kama anataka kuongeza
mchezaji mwingine nilikuwa namshauri kwamba kuna mchezaji mmoja mimemuona. Nilikuwa
namwambia mimi nimewaona wazuri sijui kama wewe utawaona wazuri, katika
wachezaji wote niliowaona kila akiwaita na kufanya nao mazoezi, jioni ananiita
na kusema kweli wewe unawajua wachezaji
Mwandishi:
Wachezaji gani ambao ulimshauri Maximo awachukue na wakafanya maajabu?
Mexime: Wapo wengi ambao walikuwa hawapewi nafasi,
mfano Ngassa (Mrisho), Boban (Haruna Moshi) walikuwa hawapewi nafasi timu ya
taifa, watu walikuwa wanapiga kelele, Maximo alikuwa ananiuliza namwambia wale
ni wachezaji wazuri. Sio hao tu, wapo wengi ambao walikuwa wadogo na mimi ndiye
niliwapokea timu ya taifa. Yeye alikuja akakuta tupo wakongwe watupu, uliona
alivyoingiza maingizo mapya.
Mimi haikuwa wachezaji wa Mtibwa tu, kama
nimemuona Simba, Yanga, sijui timu gani ana uwezo namwambia kuna mtu tukijaribu
kumuita anaweza kutusaidia
Mwandishi: Baada ya Maximo kukupa wazo la kusomea
ukocha ulilipokeaje?
Kwanza nilikuwa nimeshapanga kustaafu, wakati
nacheza ikatokea kozi Morogoro, baada ya mapumziko nikaenda kusomea, aliposikia
akaniambia umeenda kusomea, basi vizuri. Akasema endelea na tulipokuja kutolewa
na Msumbiji nikastaafu, akasema sijapenda, lakini sina jinsi, naheshimu uamuzi
wako, endelea na ukocha.
Mwandishi:
Ulikuwa na malengo gani ya muda mrefu baada ya kuingia kwenye ukocha?
Mexime: Mimi kwanza nilikuwa najifunza, unajua
wakati nacheza kulikuwa na makocha wengi, ujue falsafa yangu ipo tofauti na
makocha wengine, kipindi nacheza tulikuwa tunatumia nguvu sana, mbio nyingi,
lakini mimi nimecheza miaka ya karibuni ninajua wachezaji uishi nao vipi.
Wachezaji huwa hawapendi mbio kwenye mpira, lakini
mbio ni lazima. Ujue kuna mazoezi mengi sana ya mpira, lakini unatakiwa uyajue,
ukimkimbiza mchezaji huku anachezea mpira anafurahi na kucheka. Zoezi lile
linaingia kuliko umwambie kimbia raundi 10 au 20, mimi nadhani falsafa yangu
hapo ndipo ipo tofauti.
Kipindi cha kabla ya msimu mbio zipo, lakini
kwenye ligi tena ukipiga mbio, haifai, ujue watu wengi wanaamini sana hivyo,
mimi falsafa yangu haiko hivyo, naamini mchezaji nimuumize na mpira, nimuumiza
na mechi ndogo,ndio maana unaona kwenye timu yangu wachezaji huwa wanacheza
mpira
Mwandishi:
Fafanua falsafa yako au unaamini mpira wa aina gani?
Mimi naamini mpira ambao timu lazima icheze, sisi
tunacheza mpira, mpira kama hela, kila mtu duniani anaishi anatafuta hela,
kwahiyo ukitaka kuwa na maisha mazuri inabidi hela uitafute wewe, ukishaipata
hela inabidi uitawale ili uweze kuishi maisha mazuri.
Kuipata hela sio kazi, kazi uitawale vipi? Sasa ndio
mpira, wapo watu 22, kila mtu anautaka mpira, ndio mfano wa hela, inadibi
wachezaji wote tuutafute ule, tunapoutafuta mchezaji wetu kaupata tutautawala
vipi, sasa hapo ndipo inakuja hali ya kumiliki mpira. Hii ina mazoezi yake na
mnafanya ile kazi ya kumiliki mpira, kwenye mechi mkiwa na mpira ni rahisi
kufunga, mkiwa na mpira sio rahisi kufungwa. Hata Barcelona wakati wa Pep
Guardiola iliwashinda wengi kwasababu ya kumiliki mpira, wakipoteza wanapambana
haraka kuurudisha kwao, mkiwa na mpira ni rahisi kuwafunga watu, kwasababu ni
ngumu kuutafuta mpira.
0 comments:
Post a Comment