Ronaldo na Shayk wameripotiwa kuachana kwasababu ya mwanamitindo huyo wa Urusi kugoma kuhudhuria sherehe ya kuzaliwa ya mama yake Ronaldo
Mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo (wa pili kulia) jana jumamosi alifanya mazoezi na wachezaji wenzake
RASMI Irina Shayk amerudi sokoni, hii ni kwa mujibu wa wakala wake.
Imeripotiwa New York Post kuwa muwakilishi wa Shayk amezungumzia kuachana kwa mwanamitindo huyo na mchumba wake Cristiano Ronaldo: "Tunaweza kuthibitisha kwamba Irina Shayk amevunja mahusiano na Cristiano Ronaldo.'
Bado haijajulikana wazi chanzo cha mpasuko huo, lakini tetesi nyingi zinazunguka mahusiano mabaya ya Mwanamitindo huyo wa Urusi na mama mzazi wa Ronaldo.
Wakala aliongeza: " Alikuwa karibu sana na familia kupitia mahusiano yao. Tetesi zozote mbaya kuhusu Irina na familia ya Ronaldo ni uongo na sio sababu ya wawili hao kuachana. Kwasasa Irina hana cha kuzungumza".
Shayk aligoma kuhudhuria sherehe ya 60 ya kuzaliwa mama yake mshindi wa Ballon d'Or, kwa mujibu wa magazeti ya Ureno.
Mtu wa familia: Cristiano alisindikizwa jukwaani na mama yake mzazi, Maria Dolores dos Santos Aveiro
0 comments:
Post a Comment