Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
LIGI Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) iliingia raundi ya 12 wikiendi iliyopita huku mshambuliaji Samwel Kamuntu akionesha kuwa amepania kukinyakua kiatu cha mfungaji bora baada ya kufunga katika mechi nne mfululizo.
Kamuntu amekuwa lulu katika kikosi cha kocha mzawa Fred Felix Minziro cha JKT Ruvu Stars ambacho sasa kinakamata nafasi ya tatu kikiwa na pointi 18 sawa na Yanga SC walioko nafasi ya pili kwa faida ya tofauti nzuri ya mabao ya kufunga na kufunga, pointi tatu nyuma ya vinara Azam FC.
Mshambuliaji huyo alifunga bao lake la tano msimu huu juzi katika mechi yao ya jana waliyotoka sare ya 1-1 dhidi ya Mgambo Shooting Stars Uwanja wa Azam, Dar es Salaam.
Kamuntu alifunga pia katika mechi zote nne zilizopita dhidi ya Coastal Union FC, Stand United FC, Mtibwa Sugar FC na ya juzi dhidi ya kikosi cha Bakari Shime cha Mgambo.
Byota huyo sasa ana mabao matano sawa na Ame Ally Amour wa Mtibwa Sugar FC, Rashid Mandawa wa Kagera Sugar FC na Danny Mrwanda wa Yanga SC.
WAKALI WA KUCHEKA NA NYAVU VPL
7. Didier Kavumbagu Azam FC
------------------------------
5. Ame Ally Amour Mtibwa Sugar
Rashid Mandawa Kagera Sugar
Danny Mrwanda Polisi/Yanga SC
Samwel Kamuntu JKT Ruvu Stars
------------------------------
4. Rama Salim Coastal Union
Simon Msuva Yanga SC
Emmanuel Okwi Simba SC
------------------------------
3. Ally Shomary Sharif Mtibwa Sugar
Nassoro Kapama Ndanda FC
Kipre Tchetche Azam FC
------------------------------
2. Aggrey Morris Azam FC
Amisi Tambwe Simba/Yanga SC
Deus Kaseke Mbeya City FC
Ibrahim Hassan Tanzania Prisons
Jabir Aziz JKT Ruvu Stars
Jacob Masawe Ndanda FC
Mussa Mgosi Mtibwa Sugar FC
Najim Magulu JKT Ruvu Stars
Nicholas Kabipe Polisi Moro
Shaban Kisiga Simba SC
------------------------------
TANO ZA JUU
Na.Timu Pld W T L GF GD Pts
1. Azam 11 6 3 2 15 7 21
2. Yanga 10 5 3 2 12 4 18
3. JKT 12 5 3 4 12 1 18
4. Mtibwa 10 4 5 1 13 6 17
5 Coastal 11 4 4 3 10 2 16
0 comments:
Post a Comment