Aaron Ramsey akishangilia na Alex Oxlade-Chamberlain, Olivier Giroud na Per Mertesacker kwenye uwanja wa Etihad
Jamie Carragher amewaponda nyota wa Arsenal kwa kitendo cha kushangilia kuzidi kiasi kufuatia kuifunga Manchester City jumapili iliyopita uwanja wa Etihad.
Aaron Ramsey ali-post picha katika mtandao wa Instagram akiwa yeye na wachezaji wenzake Alex Oxlade-Chamberlain, Olivier Giroud na Per Mertesacker wakiwa katika hali ya furaha kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.
Sio huyo tu aliyekuwa 'bize' na mitandao ya kijamii kufuatia ushindi wa 2-0, naye Alexis Sanchez alijipiga picha akiwa na marafiki zake.
Alexis Sanchez (juu) alijipiga picha akiwa na Mesut Ozil, Mathieu Flamini na Oxlade-Chamberlain
Hata hivyo, kitendo hicho kimemfanya beki wa zamani wa Liverpool na England, Jamie Carragher, aamini kuwa Arsenal wanatakiwa kuacha kushangilia kupita kiasi mpaka watakaposhinda makombe kadhaa.
Carragher ali-post picha yake akiwa na mchambuzi mwenzake wa Sky Sports , Gary Neville baada ya kumaliza show, lakini aliwaambia Monday Night Football: "Inanishangaza sana---huu ni utani mkubwa.
"Ilikuwa mechi ya miamba miwili. Kiukweli unaweza kushangilia, lakini haina maana kuweka mapicha mengi namna hii ya chumba cha kubadilishia nguo. Siku zote picha zenye makombe ndio tamu, haina maana kwa mipicha hii na wanatakiwa kuacha kufanya hivyo".
0 comments:
Post a Comment