LIGI kuu Tanzania bara inaendelea kwa mechi mbili
kupigwa viwanja viwili tofauti nchini.
Wagosi wa Kaya waliofanya maandalizi makubwa
wakicheza mechi ya kirafiki na Kombaini ya Mombasa mwishoni mwa wiki iliyopita na
kutoka sare ya 1-1 kwa lenngo la kupata makali wanachuana vikali na Polisi
Morogoro.
Mechi hiyo kali inapigwa uwanja wa CCM Mkwakwani
Tanga ambapo mashabiki wa Coastal wataingia kuona namna kikosi chao
kilivyobadilika.
Mabingwa hao wa Tanzania mwaka 1988 wanaonekana
kuwa na ubora msimu huu tofauti na mwaka jana, lakini Wapinzani wao Polisi Moro
wanaonolewa na Adolf Rishard nao wamekuwa wapinzani wa kweli.
Mechi nyingine itapigwa katika uwanja wa Azam Complex
ambapo vinara wa ligi kuu, Mtibwa Sugar watakabiliana na wenyeji JKT Ruvu.
Mtibwa Sugar ambao hawajafungwa mechi yoyote mpaka
sasa wanaingia na machungu ya kutandikwa na Simba penalti 4-3 na kupokwa kombe
la Mapinduzi.
Mechi hiyo ya fainali ilichezwa januari 13 mwaka huu
uwanja wa Amaan Kisiwani Unguja Zanzibar.
Ligi kuu iliendelea jana kwa mechi tano kupigwa na
matokeo yako kama ifuatavyo:
Yanga
SC v Ruvu Shootings
|
0 :0
|
Kagera
Sugar FC v Mbeya City FC
|
0 : 1
|
Ndanda
fc v Simba sc
|
0 : 2
|
Stand
United v Azam fc
|
0: 1
|
Mgambo
JKT v Tanzania Prisons
|
0 : 0
|
0 comments:
Post a Comment