Gary Neville amemshauri kocha wa Manchester United kutumia mabeki wanne badala ya watatu
Gary Neville amemshauri bosi wa Manchester United, Louis van Gaal kuendelea kutumia mabeki wanne katika mechi zote zilizosalia msimu huu.
Mashetani wekundu walianza na mabeki watatu wa kati katika ushindi wa 2-0 dhidi ya QPR kwenye mechi ya jumamosi ya ligi kuu England, lakini walibadilisha na kuingia katika mfumo wa mabeki wanne na hatimaye Marouane Fellaini na James Wilson walifunga magoli kuipa pointi tatu Man United.
Mashabiki wa United hawapendi mfumo unaopendwa zaidi na Van Gaal wa 3-5-2 na Neville amewaunga mkono.
Louis van Gaal aliingia kwenye mfumo wa 4-4-2 katika mechi ya jumapili iliyopita dhidi ya QPR
0 comments:
Post a Comment