Tuesday, January 13, 2015

YANGA itaifungulia Simba kesi ya madai ya dola milioni moja sawa na Sh 1.7 bilioni kiasi ambacho timu ya Wadi Degla FC ya Misri nayo itatakiwa kulipa kama Yanga ikishinda kesi kwa hoja inazojenga.
Yanga inataka straika, Emmanuel Okwi raia wa Uganda asijihusishe na masuala ya soka kwa kipindi kisichopungua miaka mitano.
Pia, rungu hilo limemwangukia straika wao wa zamani, Mbrazili Genilson Santos ‘Jaja’ ambaye wanataka awalipe dola 56,000 sawa na Sh97 milioni ambapo kati ya pesa hizo, dola elfu 20 sawa na Sh 35 milioni ni fidia ya pesa za usajili alizochukua na dola 36,000 sawa na Sh63 milioni ni pesa za mshahara wa miezi 12, wakati Juma Kaseja anatakiwa alipe kiasi cha Sh300 milioni fidia ya pesa za usajili na Sh26 Mil kama sehemu ya mshahara wake wa miezi 12 ambayo imebakia kwenye mkataba wake na Yanga.
Mkuu wa Idara ya Sheria katika klabu ya Yanga, Frank Chacha, alitolea ufafanuzi wa suala hilo kwa Mwanaspoti jana Jumatatu, katika ofisi za Makao Makuu ya Klabu hiyo Jangwani jijini Dar es Salaam kuwa, yamefikia mahali pazuri na hadi kufikia mwezi Machi mambo yatakuwa yameshakamilika.
Alisema: “Suala la Okwi, tutafungua kesi ya madai Fifa tunataka afungiwe kujihusisha na shughuli za michezo kwa kipindi kisichopungua miaka mitano. Pili atulipe kiasi cha dola Milioni 1 (sawa na Sh1.7 bilioni) kama fidia ya kuvunja mkataba na dola 100,000 kwa ajili ya gharama za huduma tulizompa kama kufundishwa mazoezi na mambo mengine.
“Pia klabu zilizohusika kama Simba na Wadi Degla kila moja inatakiwa kulipa dola milioni moja (sawa na Sh. 1.7 bilioni) Wadi Gegla inahusika kwa sababu wameingilia mkataba walipozungumza na Okwi ukiwa bado mrefu, wakati Simba ndiyo klabu anayoichezea sasa, amejiunga wakati mkataba wake ukiwa mwanzoni,”alisema Chacha..
“Na Jaja ambaye alibaki kwao kwa madai ana matatizo ya kifamilia na baadaye akakaa kimya tu hadi leo hii bila taarifa yoyote na sasa kuna timu anaichezea, tutamfungulia kesi Fifa ya kumdai fidia ya dola elfu 20 (sawa na Sh35 Mil) pamoja na dola elfu 3 mara 12 (sawa Sh63 Mil) ikiwa ni sehemu ya mshahara wake kwa muda wa mwaka mmoja,”alisema Chacha.
Chacha alikwenda mbali na kulitolea ufafanuzi suala la Kaseja na kusema, watamfungulia kesi mahakama ya kazi: “Kaseja anatakiwa kuilipa Yanga Sh300 Mil, hiyo ni fidia ya kuvunja mkataba na Sh2.2 Mil mara 12 ikiwa ni sehemu ya mshahara wake kwa muda wa mwaka mmoja uliokuwa umebaki katika mkataba wake.”
Amesema, Kaseja alituma barua ya kutaka kuvunja mkataba kwa sababu ya mambo matatu ambayo ni kutomaliziwa pesa ya usajili Sh20 Mil, hakupata nafasi ya kucheza na tatu hakukatiwa bima ya majeruhi, lakini wao walimfafanulia kila kitu.
Lakini alituma barua ya kuvunja makataba Novemba 11 mwaka 2014 wakati pesa zake za usajili zilikuwa zimeshatumwa tangu Oktoba 27, 2014 kwa maana hiyo yeye ndiye alivunja mkataba.
Chacha aliendelea na kusema, watawafungulia kesi ya madai ya zaidi ya Sh100 milioni wanachama; Wema Chikota, Juma Mtibwa na Kingwamba Kingwamba ambao walifungua kesi ya kupinga katiba ya Yanga ya mwaka 2010 na kuitambua ile ya mwaka 1968
Source: Mwanaspoti

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video