KOCHA mkuu wa Simba SC, Goran Kopunovic yuko
tayari kuiongoza timu yake katika mchezo wake wa kwanza wa ligi kuu soka
Tanzania bara utakaopigwa uwanja wa CCM Nangwanda Sijaona jioni ya leo Mkoani
Mtwara.
Kwa mujibu wa Afisa habari wa Simba, Humphrey
Nyasio ambaye amezungumza na mtandao huu asubuhi hii kwa njia ya simu kutoka
Mtwara, Kikosi cha Simba hakina majeruhi yeyote na kocha amefurahishwa na hali
hiyo.
“Tuko ‘fresh’ kabisa. Jana jioni tulifanya mazoezi
na mashabiki wengi walijitokeza kutuona mabingwa wa kombe la Mapinduzi. Hii
inaashiria wanaiamini timu yao.” Amesema Humphrey. “Kocha amekiandaa kikosi
chake na ameeleza kuwa yuko tayari kwa ajili ya mechi”.
Kopunovic anapenda soka wa wazi la kumiliki mpira,
kushambulia kwa kasi na kukaba kwa umakini kuanzia safu ya kiungo na kipindi
ambacho ameiongeza Simba kombe la Mapinduzi, vijana wameonekana kuwa na
mabadiliko kiuchezaji.
Tusubiri kuona Mserbia huyu atavuna nini katika
mechi ya ligi na ikumbukwe kwamba Simba hawaja na matokeo mazuri mpaka sasa.
Katika mechi nane walizocheza, wametoka sare mechi
sita, wamefungwa moja na kushinda moja.
0 comments:
Post a Comment