Shirikisho la Soka duniani, FIFA,
limesema vilabu vya mpira wa miguu vilitumia kiasi cha dola bilioni nne
nukta moja katika uhamisho wa wachezaji wa kimataifa mwaka uliopita,
ambacho ni kiwango cha juu kabisa kuwahi kufikiwa katika uhamisho wa
wachezaji.
Uingereza ndiyo iliyotumia kiasi cha juu kabisa duniani, kwa timu zake kulipa dola bilioni moja nukta mbili mwaka 2014.
Vilabu vya Hispania vilishika nafasi ya pili kwa matumizi ya uhamisho wa wachezaji, vikitumia dola milioni mia saba.
Takwimu
hizo pia zinabainisha kuwa India ilisajili wachezaji wenye umri mkubwa
kuliko wote duniani kwa wastani, na China ikiingia katika kundi la nchi
kumi za kwanza katika matumizi ya uhamisho kwa mara ya kwanza katika
historia ya nchi hiyo.
Takwimu hizi mpya hazihusishi uhamisho wa wachezaji kati ya timu moja na nyingine ndani ya nchi husika.
0 comments:
Post a Comment