Friday, January 16, 2015

Wachezaji wa Yanga wakifanya mazoezi leo uwanja wa Boko Veteran

YANGA itawakosa Mbuyu Twite na Nadir Haroub ‘Cannavaro’ katika mechi ya kesho ya ligi kuu soka Tanzania bara itakayopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam dhidi ya Ruvu Shootings.
Twite ana majeruhi ya goti aliyopata katika mazoezi ya timu hiyo katikati ya wiki hii, wakati Cannavaro anamalizia adhabu yake ya kufungiwa mechi tatu.

Licha ya kuwakosa wachezaji hao muhimu wa kikosi cha kwanza, kocha mkuu wa Yanga, Mholanzi, Johannes Hans van der Pluijm amesema wana matarajio makubwa ya kupata ushindi kwani kwa wiki nzima wamefanya mazoezi ya ufundi.

Moto ukiwa umekolea katika mazoezi ya Yanga leo

Akizungumza katika mazoezi ya Yanga yaliyofanyika leo uwanja wa Boko Veteran, Pluijm anayependa mpira wa wazi na kushambulia kwa kasi amesema nafasi ya mabeki wa kati atawaanzisha Rajab Zahir na Kelvin Patrick Yondani.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video