TUNISIA wanaanza kampeini zao leo za kusaka ubingwa wa kombe
la Mataifa ya Afrika, Afcon 2015 kwa kukabiliana na Cape Verde katika mechi ya
kundi B itayopigwa uwanja wa Nuevo Estadio majira ya 4:00 usiku kwa saa za
Afrika mashariki.
Wakati miamba hiyo ya soka kaskazini mwa Afrika ikiingia
uwanjani kama moja ya timu inayopewa nafasi ya kutwaa ubingwa kufuatia kampeini
nzuri wakati wa mechi za kufuzu, Cape Verde wanaingia uwanjani kama wachanga
kabisa.
Hata hivyo Cape Verde ‘Blue Sharks’ ambao wanashiriki kwa
mara ya pili Afcon (walishiriki kwa mara ya kwanza 2013 nchini Afrika kusini na
kuonesha kiwango cha juu), wamekuwa miongoni mwa nchi zilizoendelea kwa kiwango
cha juu kisoka duniani miaka miwili au mitatu iliyopita.
Mechi ya
mapema itayoanza majira ya saa 1:00 usiku inawakutanisha Zambia dhidi ya DR
Congo.
MATOKEO ZA MECHI ZA JANA KUNDI A HAYA HAPA:
MECHI
|
MATOKEO
|
Guinea ya
Ikweta v Congo Brazaville
|
1
: 1
|
Burkina Faso
v Gabon
|
0
: 2
|
0 comments:
Post a Comment