UKURASA mpya utaandikwa katika historia ya soka la Afrika pale
atakapopatikana mchezaji bora wa Afrika kwa mwaka 2014.
Kuna historia inayowazunguka wachezaji watatu wanaopewa nafasi
kubwa ya kutwaa tuzo hiyo; mshambulaiji wa Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang,
golikipa wa Nigeria Vicent Enyeama na kiungo wa Ivory Coast Yaya Toure.
Wachezaji hao watatu wote walikuwa na msimu mzuri katika timu zao
za taifa na klabu zao na kuwafanya wakaribiane zaidi kutwaa tuzo hiyo. Kila
mmoja anastahili kupewa tuzo ya Mwanasoka bora wa Afrika.
Toure, mshindi wa tuzo hiyo mara tatu mfululizo anakabiliana na
upinzani mkubwa kutoka kwa Aubameyang na Enyeama katika harakati zake za kutaka
kutwaa tuzo hiyo kwa mara nne mfululizo.
Nyota wa zamani wa Cameroon, Samuel Eto’o ndiye mchezaji pekee
aliyeshinda tuzo hiyo mara nne -mwaka 2003, 2004, 2005 na 2010.
Toure ndiye mchezaji anayetaka kuifikia rekodi hiyo ya Eto’o,
lakini pia anahitaji kuwa mchezaji pekee aliyetwaa tuzo za mwanasoka bora wa
Afrika mara nne mfululizo.
Aubameyang na Enyeama pia wana rekodi zao walizoweka. Nyota huyo
wa Gabon atakuwa mchezaji wa kwanza wan chi hiyo kutwaa tuzo hiyo ya heshima
tangu mwaka 1992.
Kama Enyeama atashinda tuzo
hiyo atakuwa golikipa wa kwanza kufanya hivyo. Pia atakuwa Mnigeria wa kwanza
kutwaa tuzo hiyo tangu mwaka 1999.
Mshambuliaji Gwiji wa Nigeria, Nwankwo Kanu ndiye alikuwa Mnigeria
wa mwisho kutwaa tuzo hiyo mwaka 1999. Wanigeria wengine walioshinda tuzo hiyo
ni Rashidi Yekini (1993), Emmanuel Amunike (1994) na Victor Ikpeba (1997).
Enyeama
Kwa upande wa mchezaji bora wa Afrika anayecheza soka la ndani,
waalgeria wawili, Akram Djahnit na El Hedi Belamieri watapambana na mshambuliaji wa DR Congo,
Firmin Mubele Ndombe. Mshindi atapatikana kwa kura zitakazopigwa na Makocha
wakuu au wakurugenzi wa ufundi wa vyama wanachama wa CAF.
Shoo hiyo ya kumpata mwanasoka bora wa Afrika itafanyika kwa
dakika 180 na sherehe hizo zitatumbuizwa na wanasanii wakubwa wa Afrika.
Mapacha wawili wa Hip Hop, P-Square watatoa burudani kali mbele ya
umati wa watu watakaohudhuria sherehe hizo.
Pia Lagbaja
atatumbuiza sambamba na wasanii wengine kama vile Fally Ipupa; global Jazz
icon, Hugh Masekela kutoka Afrika
kusini, mwimbija wa Misri, Hakim.
Wasanii
wengine ambao watatumbuiza katika shoo hiyo itakayooneshwa moja kwa moja duniani
kote watakuwa ni Soweto Gospel Choir kutoka Africa kusini, kundi la kwaya la Uhuru;
pan African group, Cirque D’Afrique na nyota wa muziki Tanzania, Diamond
Platinumz.
HAPA CHINI NI ORODHA YA TUZO MBALIMBALI ZINAZOWANIA BARANI AFRIKA
MCHEZAJI BORA WA AFRIKA (wamepangwa
kwa kufuata alphabeti)
Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon na Borussia Dortmund)
Vincent Enyeama (Nigeria na Lille)
Yaya Toure (Cote d’Ivoire na Manchester City)
MCHEZAJI BORA WA AFRIKA-Anayecheza
soka Afrika
Akram Djahnit (Algeria na ES Setif)
El Hedi Belamieri (Algeria
na ES Setif)
Firmin Mubele Ndombe (DR Congo na AS Vita)
MCHEZAJI BORA WA AFRIKA WANAWAKE
Annette Ngo Ndom (Cameroon na Amazon Grimstad)
Asisat Oshoala (Nigeria na River Angels)
Desire Oparanozie (Nigeria na Guingamp)
MCHEZAJI BORA AFRIKA KIJANA
Asisat Oshoala (Nigeria na River Angels)
Fabrice Ondoa (Cameroon na Barcelona)
Uchechi Sunday (Nigeria na River Angels)
MCHEZAJI BORA ANAYECHIPUKIA
Clinton N’jie (Cameroon na Olympique Lyon)
Vincent Aboubakar (Cameroon na Porto)
Yacine Brahimi (Algeria na Porto)
KOCHA BORA WA MWAKA
Florent Ibenge (DR Congo)
Kheireddine Madoui (ES Setif)
Vahid Halilhodžić (Kocha wa zamani wa Algeria)
TIMU BORA YA TAIFA YA MWAKA 2014
Algeria
Libya
Nigeria
TIMU BORA YA TAIFA YA WANAWAKE YA
MWAKA
Cameroon
Nigeria
Nigeria U-20
KLABU BORA YA MWAKA
Al Ahly (Egypt)
AS Vita (DR Congo)
Sewe Sport (Cote d’Ivoire)
MWAMUZI BORA WA MWAKA
Alioum Neant (Cameroon)
Doue Noumandiez Desire (Cote d’Ivoire)
Papa Bakary Gassama (Gambia)
KIONGOZI BORA WA MPIRA WA MWAKA
Moise Katumbi Chapwe – Rais wa TP Mazembe (DR Congo)
TUZO YA GWIJI WA AFRIKA
Oryx Club (Cameroon) – winners of the maiden edition of CAF
Champions League 1964
Stade Malien (Mali) - runner
up of the maiden edition of CAF Champion’s League 1964
0 comments:
Post a Comment