Wednesday, January 28, 2015

YAYA Toure hachezi kwa kiwango cha juu anapoitumikia Ivory Coast katika michuano ya Afcon 2015 inayoendelea Guinea ya Ikweta ukilinganisha na anavyocheza akiwa Manchester City kwasababu kuna wachezaji wenye ubora tofauti, amedai kocha Herve Renard jana.
Nahodha huyo wa Tembo wakati wote ameonekana kuwa chini ya kiwango huko Guinea ya Ikweta akishindwa kuisaidia timu kupata ushindi katika mechi mbili za kundi D.
"Ivory Coast sio Manchester City. Ubora wa wachezaji haufanani," Amesema kocha huyo mzawa wa Ufaransa kuelekea mechi ya mwisho ya kundi D dhidi ya Cameroon dimba la Malabo leo usiku.
"Pale City, kuna wachezaji ambao wanaweza kulinda vizuri na kutengeneza nafasi kwa wakati mmoja. Kwetu sisi ni tofauti, kwahiyo tulimuomba afanye majukumu mengine"

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video