Kocha wa klabu ya Liverpool Brendan Rodgers amemmwagia sifa
kedekede mlinda mlango wa Chelsea Thibaut Courtois na kusema ndio mchezaji bora katika mchezo wao wa kombe
la Capital One uliopigwa jana katika dimba la Stanford bridge.
Rodgers
alisema licha ya timu yake kufanya jitihada zote kuhakikisha inachomoza na
ushindi katika mchezo huo na mpaka kufika dakika za nyongeza mia ishirini,
golikipa huyo raia wa ubelgiji ndio aliwanyima ushindi kwa kulinda lango lake
kwa ustadi wa hali ya juu.
“Hakuna shaka
Courtois ndio alikuwa mchezaji bora katika mchezo wa jana licha ya bao pekee
kufungwa na beki wa pembeni Branislav Ivanovic katika dakika za nyongeza”alisema
Brendan Rodgers.
Chelsea sasa
imefanikiwa kutinga fainali ambapo itapambana na mshindi kati ya Tottenham
Hotspurs au Sheffield United zinazoshuka ugani usiku wa leo kutafuta tiketi hiyo kwenda wembly.
0 comments:
Post a Comment