Wednesday, January 28, 2015

Boniface Wambura,Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF.

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limesema linachukukizwa na vitendo vya baadhi ya wachezaji kupiga marefa viwanjani lakini linatoa adhabu ndogo kwa wahusika kutokana na kanuni mbovu zilizopendezwa na wadau wa mchezo huo nchini.
 
Wiki iliyopita TFF ilitoa adhabu ndogo ya kumfungia kucheza mechi tatu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) na kumpiga faini ya Sh.500,000 winga Haroun Chanongo wa Stand United baada ya kupatikana na hatia ya kumpiga teke refa wakati wa mechi yao ya ligi hiyo dhidi ya Polisi Moro mjini Morogoro Januari 3, adhabu ambayo imekosolewa kwamba haimfanyi mtu kujutia alichokifanya.
 
Katika mahojiano na NIPASHE jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Boniface Wambura, mkurugenzi wa mashindano wa shirikisho hilo, alikiri kuwa Kanuni Na. 37 ya Kanuni za Ligi za TFF toleo la 2014 (Adhabu za Wachezaji Wanaofanya Vurugu Viwanjani) haina mashiko ikilinganishwa na fedheha ambayo marefa wanaopigwa wamekuwa wakiipata.
 
Wambura alisema awali walikuwa na kanuni kali kwa watu wanaojihusisha na vurugu viwanjani, lakini kanuni hizo zilibadilishwa misimu miwili iliyopita kutokana na mapendekezo ya wadau wa soka zikiwamo klabu za Ligi Kuu.
 
2009 hadi 2013 Kanuni ya 25 ya Kanuni za Ligi za TFF ilitamka wazi kwamba mchezaji anayepiga refa na maofisa wa mechi atafungiwa kujishughulisha na mpira wa miguu kwa muda wa miezi 3 hadi 12 na kupigwa faini nyingine inayopendekezwa na Kamati ya Utendaji ya TFF kwa kuzingatia matakwa ya iliyokuwa Kanuni ya 31 ya Kanuni za Ligi za TFF.
 
"Sisi (TFF) tulikuwa na adhabu kali kwa wachezaji wanaowafanyia vurugu marefa viwanjani. Baada ya kutoka adhabu ya kuwafungia mwaka mzima baadhi ya wachezaji misimu miwili iliyopita (Stephano Mwasika), wadau walikosoa kanuni hiyo na kupendekeza kuwa na adhabu iliyopo kwa sasa (mechi 3 faini ya Sh. 500,000).
 
"Tulitaka kuwe na adhabu kali zaidi za kuwafungia kwa muda mrefu maana mchezaji wa Simba kwa mfano kumpiga faini ya Sh.500,000 haiwezi kumuuma na kujutia kosa kwa sababu pesa yenyewe analipiwa na klabu.
 
"Lakini wadau walitukosoa wakisema kumfungia mchezaji mwaka mzima kunaua kipaji chake ndiyo maana tukawa na adhabu ndogo ambazo leo zinaonekana kukosolewa," alisema zaidi Wambura.
 
Januari 25, 1995 aliyekuwa nahodha wa Manchester United, Eric Cantona alifungiwa na Chama cha Soka cha England (FA) kucheza soka miezi nane na kutozwa faini ya paundi 30,000 (Sh. milioni 79) kwa kumpiga teke shabiki wa Crystal Palace Matthew Simmons aliyekuwa jukwaani.
 
Cantona alioneshwa kadi nyekundu baada ya kumpiga teke beki Richard Shaw wa Palace baada ya beki huyo kumvuta shati. Wakati akitoka uwanjani, Cantona alivamia jukwaa la mashabiki na kumtwanga teke la mtindo wa kung-fu shabiki Simmons kwa madai kwamba shabiki hayo alitoa matusi yaliyomlenga mama wa nyota huyo wa zamani wa United.
 
United walijaribu kusaka mbinu za kumuuza na kumuondoa katika Ligi Kuu ya England (EPL) ili akacheze nchi nyingine lakini Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) likaawambia adhabu ya kifungo ingekuwa pale pale hata kama angehamia katika ligi nyingine.
 
Katika kuhakikisha kwamba tukio hilo halijirudii, Shirikisho la Soka la Ufaransa (FFF) lilitoa adhabu pia kwa kumvua Cantona unahodha wa timu ya taifa ya Ufaransa na hakuitwa tena katika kikosi hicho hadi alipostaafu soka.
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video