Chicharito
Klabu ya Lazio inayoshiriki ligi kuu nchini Italia almaarufu
kama Serie A imeonyesha nia ya kumsajili mshambuliaji wa klabu ya Manchester United
anaekipiga katika klabu ya Real Madrid kwa mkopo na timu ya taifa ya Mexico
Javier Hernandez almaarufu kama Chicharito.
Lakini bado mabingwa watetezi wa kombe la klabu Bingwa Barani Ulaya Real Madrid chini ya kocha Carlo Ancelloti wanasita kumtoa
mchezaji huyo mpaka mwisho wa msimu.
0 comments:
Post a Comment